Basi angetembea na mwanamke mwingine sio Judy rafiki yangu!

ndyoko

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,971
Reaction score
1,652
Asalam aleykum wanJF!

Ni juzi kati shemeji yangu (Editha-sio jina halisi) alikuja nishtakia kuwa BF
wake wa zamani (Erick-sio jina halisi) mpiga chini. Cahnzo ni kuwa Erick
hakuwa na hela wakati huo.

Hata hivyo kwa sasa Erick mambo yake ni safi na mdada baada ya kutemwa
na BF mpya ameanza kutamani kurudia urafiki wake na Erick. Hata hivyo
Erick tayari amaeanza uhusiano na Judy ambaye ni rafiki wa Editha.

Sasa lawana za Editha ni kwamba yeye bado anampenda Erick na inamuuma
kuona anatembea na Judy ambaye ni rafiki yake. Sasa amekuja kwangu akidai
eti nijaribu kumuombea msamaha kwa Erick warudiane, na kama haiwezekani
basi nimshawishi asitembee na Judy kwa sababu Judy ni rafiki yake.

Kila siku Editha amekuwa akinipigia simu kujua kama ujumbe wake
nimeshauwasilisha kwa Erick. Binafsi sijauwasilisha ingawa huwa
namyeyusha kuwa tayari nimeshafanya hivyo.

'Sasa shemeji kama umemwambia mbona bado wako wote? Kama ni mwanamke
"Basi angetembea na mwanamke mwingine sio Judy rafiki yangu!".

Note: Hivi kuna kosa kutembea na rafiki wa mpenzi wako aliyekutema mwenyewe?
Kinachomfanya mtu aumie ni nini 'unapotembea' na rafiki yake ili hali
mwenyewe ndo alokutema?
 
Huyo shemeji yako ni chizi miwaya, umeshapigwa chini, rafiki nae kajipanga hapo hapo. Kwanini hakai akatafakari kama huyo jamaa anamatatizo maana hata respect hana ya kuwachanganya yeye na rafiki yako. Maana jamaa kaona wote ni cheap ndio maana awepanga hivyo.

Kama anajipenda na kujiheshimu zaidi, kuomba kurudiana nae ni sawa na recipe for disaster!
 
Huyu Edith anamatatizo, si alimtema jamaa?
Basi atulie jamaa yuko huru kudate na mtu mwingine labda Judy ndiye alikuwa mfariji wa jamaa alipokuwa apeche na alikuwa anampa company.

Mh na Judy naye vipi kwani alikuwa anamendea jamaa ya rafikiye.lol!
 
ebwana wee mapenzi yenyewe full usanii wacha mwana amege tuu ata huyo rafiki judy lol editha akubali kuwa ndio ilishakula kwake yeye tingisha kiberiti akubali matokeo
 
Mi nina mtazamo wa tofauti kidogo. Huyo dada alifanya kosa akapigwa chini na ni wazi inaonyesha kuwa ni mtu wa tamaa ya pesa. Hana Mapenzi ya kweli.

Lakini pamoja na makosa ya huyo dada, pia siungi mkono suala la huyo kaka kuamua kutembea na aliyekuwa rafiki wa huyo gelfriend wake. Si jambo la kistaarabu kabisa ndani ya jamii kuanzisha urafiki wa kimpaenzi na ex wa rafiki yao hata kama wamegombana wao wenyewe na ugomvi ulikuwa haukuhusu. Ni sawa na kumfunua nguo rafiki yako! Na zaidi ya hapo, Mara nyingi saula kama hili huleta picha mbaya ktk jamii na kuilazimisha jamii kuhisi kuwa huyo mhusika mpya anaweza kuwa alikuwa na mahusiano na huyo aliyekuwa shemeji yake kabla ya hata rafiki yake kumwagwa au laa alikuwa akimtamani shemejiye. Nafikiri ni vyema kuwa waangalifu kuepeka migogoro kama hiyo.

Kwa ushauri kaka, huyo dada endelea kumpotezea kwa kumjibu kuwa ujumbe umefika ila wenye maamuzi ya kuachana ni wao wenyewe. Mara nyingine si jambo zuri kuingilia mahusiano ya wawili.
 
tatizo mademu wa siku nhizi wanabeep sana sasa kama Edith aliamua kutosa jamaa kinamuuma nini tena? au tamaa ya pesa? acha hizo! tena ningelikuwa mimi ningemchukua mdogo wake kabisa!!!!!!!!!
 
wote watatu hawatulia walikuwa wanatamaniana tokea zamani, kwa nini uchukue shemejio? na wewe shemeji kwa nini ukubali? tayari hapo urafiki umekufa
 
wakati mwenzake hana hela akamkimbia..mambo safi anataka kurudi...wanawake bana....
 

Horsepower, do you believe in true love?

Ulishaexperience hiyo kitu? Sio ya kulearn kumpenda mtu,, ile ya kuja automatically?

mara nyingi hiyo huwa haiangalii vitu vya nje vingine vyote, na uombe Mungu isitokee kwa kichaa.

Sisemi kuwa huyo kaka amefall kwa huyo Judy that way, huenda amejifunza kumpenda na hivyo angeweza kuavoid kumpenda. lakini kama imetokea automatically; kwangu mimi hastahili lawama.

Points zako zingine zote nakubaliana nazo!
 

Hapo kwenye red mi naona anakutaka wewe ila anaona atumie gia hiyo, au we hujagundua hilo?
 

Kaunga unamaanisha huyo amefall in love automatically na ex gelfriend wa rafiki yake? Inawezakana kweli?! au katumia kama njia ya kulipiza kisasi kwa ex wake? Umewahi kuuhisi uchungu wa kufanyiwa hivyo? Hivi kwa nini nisihisi kuwa rafiki yangu kanisaliti? Watu wote nje asiwaone mpaka huyo ex wangu?
Kaunga mdogo wangu una moyo mzuri sana kama kweli unaweza kufanyiwa hivi na rafiki yako na ukachukulia poa. Mimi siwezi, kamwe!!!
 
Mjerumani huyu anasema hivi..
Gravitation is not
responsible for people falling
in love.~
Albert
Einstein
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…