Basi la Bright Line Mwanza - Dodoma kwa hili nawapa kongole

Basi la Bright Line Mwanza - Dodoma kwa hili nawapa kongole

Doyi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2011
Posts
1,578
Reaction score
1,894
Ni gari namba T683DZE aisee kama mmepewa mafunzo huko kazini basi mmeyaelewa vyema maana TV mmeweka sauti ya chini kiasi kwamba abiria hata kusinzia unaweza kusinzia na kuifanya safari yako kuwa murua kabisa.

Screen za tv zipo saba lakini utulivu ndani ya bus upo wa kutosha. Mabasi mengine sasa hivi ningekoma kwa sauti za juu za kina Mkojani na Ngoma Nagwa au bongo fleva bila kusahau muvi za kutafsiriwa kwa kiswahili.

Kuna haja baadhi ya makampuni yaige utamaduni huu maana abiria tulio wengi tunapenda utulivu tuwapo safarini.

NB: Sina interest zozote za kibiashara au kuwaponda wengine ila panapobidi kutoa sifa tunatoa na panapo mapungufu tukosoe kwa dhamira ya kujenga zaidi.

Mimi ni abiria mwandamizi tu
 
Kwa nini usinzie kwenye bus
Kwa wadau wengine kusafiri ni sehemu ya starehe kwao. Kutuliza akili, nk. Hivyo ni jambo la kawaida kwao kusinzia.

Ni tofauti na wale abiria wa vijijini ambao wanasafiri kwa ajili ya kupeleka taarifa fulani Halmashauri (Bomani), au kwenda mjini kununua/kuuza bidhaa na baadaye kurejea kijijini.

Abiria wa aina hii utawakuta muda wote wametoa macho kama bundi.
 
Kweli kabisa umeongea
 
Afiora inayokwenda Kigoma iko hivyo pia. Ila usithubutu kutuma mzigo kwa kutumia kampuni hii (Afiora), narudia usithubutu, walah kama mzigo wako ukiwapendeza watendaji wa bus hili (Afiora) huupati kamwe. Utaambiwa buti ilifunguka ukaanguka, tugawane hasara. Kwa ufupi kampuni ile imejaa wezi, kitengo cha mizigo.
 
Back
Top Bottom