BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Tumefika Manyoni Stendi, wenye basi wakaanza kutulazimisha abiria tushuke wote ndani ya basi wakidai kwamba gari limeharibika.
Tulipohoji kipi kilichoharibika wakati kila kitu kinaonekana kipo sawa, hawasemi, abiria tukagoma kushuka.
Baadhi ya abiria wakaenda kuwafuata Trafiki kuja kusuluhisha, alipofika hapo huyo Trafiki naye anatuambia hilo basi huwa ndio kawaida yao wakifika maeneo hayo kama hawan abiria wengi ndani wanawashusha na kuwafaulisha.
Kama hii ni tabia yao na Askari wanawachekea, hii ni hatari! Jeshi la Polisi na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) wanatakiwa kuchukua hatua la sivyo ipo siku abiria watagoma kabisa kushuka na mambo yatakuwa magumu.
Baada ya mzozo wa muda mrefu wametuhamishia kwenye gari lingine la Al _ Jabry Safaris ambalo ni dogo na abiria tumebanana, kwa ufupi ni kero kubwa.
Abiria tulivyobanana baada ya kufaulishwa