Basi la Klabu ya Simba lapata ajali Zambia baada kugongana na Lori

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Basi la klabu ya Simba SC, Wekundu wa Msimbazi, ambalo lililokuwa limewabeba wanachama na mashabiki wa timu hiyo kutoka Tanzania, likielekea mjini Ndola, limepata ajali baada ya kugongana na Lori maeneo ya Kapiri Mposhi nchini Zambia.

Kwa taarifa za awali haikufahamika mara moja chanzo cha ajali hiyo huku mashabiki na wanachama wakiwa wapo salama hakuna aliyeumia zaidi ya uharibifu wa gari hilo.

Simba SC itaingia uwanja wa Kalampa Kitwe nchini Zambia Jumamosi Disemba 15, 2018 kucheza na Nkana FC katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
 
Hahaaa!! Pole sana
yaani simba kwa kuendekeza ushirikina hawajambo, onaaa sasaaa mashabiki maandazi na wanachama walikuwa watolewa naniii ili litim lao la ovyo ovyo lishindee..................
 
Kuna mijitu inaishi zama za giza. Eti kafara my foot. Huyu mjinga wanadamu wenzako wanapata ajali unahusisha na upumbavu wako na uvivu wa kufikiri.
Miaka ya nyuma aliyekua mwenyekiti wa mikia mzee juma salum alipata ajali na kufa akiwa anatokea dodoma,miaka ya juzi mafisango alipata ajali na kufa,mwaka juzi mashabiki wa simba wa tawi la mpira pesa wakiwa njiani kuelekea shinyanga kuangalia mechi ya mikia walipata ajali na baadhi yao kufariki dunia,mwaka jana jonas mkude alipata ajali akitokea dodoma kwenye mchezo wa fainali ya fa kati ya mikia na mbao,mwaka huu adam salamba mchezaji wa mikia alipata ajali na gari yake aina ya toyota crown kuharibika,na hii iliotokea huko zambia ndio yale yale yasemwayo
 
Private Mtema naye.Na kuna kiongozi wao akiitwa Ba Mchawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…