-Basi la mashabiki lililoenda Lesotho kuisapoti timu yetu ya Tanzania kwenye mchezo kufuzu Afcon 2019 kupitia Mbeya hadi Afrika Kusini sasa limegeuka basi la Walevi na wafanya Starehe. Basi hilo limeondoka Lesotho siku ya Jumatatu hadi sasa bado halijafika jijini Dar. Ikifika usiku kituo cha kupata chakula wanakaa hata masaa hata 7 wanakula, wanakunywa wanavyojisikia na wengine wanaenda Disco.
-Basi hilo limeingia Tanzania jana ila mwendo wa kutuka Tunduma hadi mbeya wanafanya wanajisikia ili hali kuna baadhi ya watu ambao ni waandishi wa habari wapo kwenye hilo basi na walikuwa na muda maalumu wa kurudi kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi ila kiongozi wa msafari naye ameingia kwenye mkumbo wa mashabiki na analifanya gari la taasisi kama mali yake ambaye imebeba walevi akiamua hata asimame mwanjela anunue Heiken Moja (mfano tu) sawa tu kwa kuwa yeye ni mkuu wa msafara.
Source: Yossima