Basi za Udart ziko wapi???

Basi za Udart ziko wapi???

Songambele

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2007
Posts
4,710
Reaction score
2,587
Tukikumbuka ahadi za wanasiasa na siasa zao uhsusani kipindi hiki cha uchaguzi tunamalizia ni watu wale wale na mambo yale yale. Nakumbuka wakati ule waziri kama sikosei Bashungwa alipiga mpaka ziara katika mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam. Ukiwa mgeni unaweza fikiri wako serious kumbe ni watu wale wale, Kipindi cha Jiwe kidogo tuliona mwanga na kudhani watumishi na wanasiasa watajifunza lakini bado ni watu wale wale.

Basi za Udart ni chache na hazipo barabarani kwa idadi ile tuliyohadithiwa wakati wanazindua mradi. Pasi na shaka miundo mbinu itakuwa mdhungu katoa hela na kasimaia mwenyewe kwa kiwango flani inaonekana na dhamira yao hakuna asiye sadiki. Kama ilivyodesturi wamatumbi walijipiga kifua mambo ya kuleta Mabasi waachiwe wao, haki ya Mungu mbwa hawa wanatutesa sana wakazi wa hili jiji kwa misongamano na kusubiri hizi gari kwa muda mrefu mno.

Kama wameshindwa kuleta mabasi yenye yatatufaa basi waruhusu daladala zetu zitumie barabara hizi mpaka watakapo pata basi. manake hata hizi basi tunazotumia ukizitazama vizuri hazikuandaliwa maalum kwa ajili ya jiji la Dar es Salaam lenye joto. Kama wameagiza mengine tafadhali wakumbuke Dsm ni joto kali na tunashindiliwa kama viazi.

Mabasi hayatoshi kunawakati Mbezi unasubiri gari mpaka saa 2 au 3 na likifika ni msongamano wa kufa mtu. Tunona jitihada zinazoendelea kupanua miundombinu lakini tunasisitiza hawa wanaondesha sasa wasifikiriwe kabisa kupewa kandarasi ya kupeleka uzoefu wao mahali kwengine. Mbwa hawa sasa hivi wanataka chenji kamili sijui wanazokusanya wanampelekea nani asiye na akili ya kujua biashara itaendelea tena kesho akabakisha chenji. Achilia mbali kutumia kadi kungemaliza kabisa huu ujinga wa chenji.

Tunajua huu ni mwaka wa kusifia watawala, please la Mwendo kasi msiwasifie watuboreshee kwa kutuongezea idadi ya Mabasi. Wanaojenga miundo mbinu wanaonekana kabisa wanajua nini wanataka, mnaowapa kandarasi ya kuendesha sasa wao hawajui kabisa nini wanataka. Ebu tununulieni hata ya Mitumba mtupunguzie hii kadhia.
 
Hao hakuna wanachoweza simamia kwa UMAKINI, sio Udart tu..angalia shirika la Ndege,Uwanja wa Mkapa,Kivuko cha Ferry Kivukoni na hata Busisi,.mfuko wa PSSSF..yaani VULULU VULULU
 
Back
Top Bottom