linapokuja suala la adhabu ya kifo tunaweza kusema si wote waliohukumiwa ni wahalifu.Siamini kama walioko jela wote ni wahalifu
Siyo sisi.....semea nafsi yako.[emoji16]Sasa sisi tufanyaje!?
Sanasana inawezekana hawa walikuwa maadui zake.Jk yupi unayemzungumzia... Tafuta rafiki yake hata mmojja km kaguswa....
Sasa sisi tufanyaje!
Pole zake hata hivyo, amefanywa tu kondoo wa Pasaka kupisha upepo upite
Pole sana mangi lazima utakuwa unatoka Rombo kwa wakina Massawe!! Huyo Mramba anatakiwa arudishe mabilioni yetu alaiyotuibia miaka yote aliyokuwa waziri; ama sivyo serikali ikamate precision Air kwani ndiko alikowekeza fedha zetu!!
Ndinani;
Si kila anayeandika humu ni mangi. Ila nakusikitikia sana weye ambaye unapika majungu kila kukicha. Kama weye una uhakika kiasi hicho mpaka unajua fedha yako iliko, basi tutakushangaa sana kuziangalia mali zako wala usifanye chochote. Pole sana ila nakushauri uchukue kikapu ukawaambie hao Precision wakupe mgao wako. Akili zingine jaman, sijui ni za perege au sato
Skuitegemea kuwa utakubali kuwa wewe mrombo lakini ukeli ndio huo ; huyo mzee ni mwizi wa muda mrefu na Mungu anamlipiza hapa hapa duniani kwa kututukana kuwa liwe na lisiwe ANGENUNUA NDEGE YA BOSI WAKE HATA INGEBIDI TULE MAJANI, yote hiyo ilikuwa kufukuzia 10% yake !! Mungu si Athumani akapigwa miaka jela na sasa anafagia pale hospitali Sinza na bahati yake ametolewa kapewa kifungo cha nje.
Kuhusu hizo fedha alizotuibia na kuwekeza huko kwenye ndege, laana itamuandama yeye na ukoo wake na hawata kaa wazifaidi kwa amani huku watoto wetu wakisoma juu ya matofali! Amekwisha pata doa maishani na hata kuwa na amani tena katika uhai wake.
Hivyo, ili kutugilib siye ambao hatukufanikiwa kuyala matunda hayo unashabikia tuamini kuwa yale majizi makuu ya awamu hiyo yalifungwa ka Mramba na Yona
Kwa hiyo yeye professional yake ni kupiga deki na kufagia?MRAMBA AELEZEA MAISHA YA JELA NA FAIDA ZA KIFUNGO CHA NJE
Aliyekuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya awamu ya tatu, Basil Mramba, ameishauri Serikali kuhakikisha inawatumia wafungwa kutumikia jamii badala ya kuwarundika magerezani kwani maisha ya gerezani si salama na si njia pekee ya kumrekebisha mhalifu aliyehukumiwa na mahakama.
Kutokana na hali hiyo, alisema kuna haja kwa Serikali kuanza kutumia sheria namba 6 ya huduma kwa jamii kuwaangalia wafungwa wenye taaluma kutumika adhabu zao katika fani au taasisi za umma ili kupunguza gharama kuwahudumia watu ambao wanaweza kuisaidia jamii.
Mramba alitoa kauli hiyo jana, wakati yeye na mwenzake aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, walipomaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza Palestina, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kutumikia adhabu ya kifungo chao cha nje baada ya wiki iliyopita Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuridhia kuwa wanastahili kutumikia jamii kwa kipindi cha miezi sita hadi Novemba 5.
“Jamii inaamini jela ni sehemu salama na mtu akishikwa na hatia kwa kosa lolote, mahala sahihi ni jela tu, kule anakutana na watu wa kila aina, wenye makosa tofauti, hali ambayo inamfanya ajifunze mambo mengine mapya.
“Unakuta mtu amefanya uhalifu wa kuiba kitu, anafungwa na kupelekwa gerezani, anakutana na majambazi sugu wanaompa mbinu zaidi, sasa akitoka jela anakuja akiwa ameiva, anarudia kwenye matukio akiwa amekamilika,” alisema Mramba.
Chanzo Dar 24
Lakini wale waliopiga za escrow wapelekwe kwanza lupangokweli hii ni point, watu wanalundikwa kule kwa gharama kubwa, hadi wanakosa nafasi hata za kusimama, wakati kuna kazi kibao za kufanya
kazi sio za kufanya usafi tuu, kuna mitaro ya maji hapa dar ya kuzibua, mvua Ikinyesha shida zipungue, majalala ya kuweka sawa, pia serikali ingeanzisha mashamba makubwa ya umwagiliaji yenye fence na ranch halafu hawa wafungwa wakaenda kutumikishwa huko, kulundika wahalifu sehemu moja halafu hawafanyi kazi bali ni kupiga soga kweli ni kuzidi kuwaongezea mbinu
Nawewe subiria ukatumikie lupango maana muda wako unakaribiaSasa sisi tufanyaje!?
Bado zamu yake sasa akaonje lupangoJk hakuwaga na mchezo kabisa.....
Waziri wa fedha mzima akala mvua,,,,,,,,,
Jk yupi unayemzungumzia... Tafuta rafiki yake hata mmojja km kaguswa
unasifia jk bila aibu kabisaJk hakuwaga na mchezo kabisa.....
Waziri wa fedha mzima akala mvua,,,,,,,,,