Bei walizokupa jamaa hapo juu ni sahihi kabisa,kwa nyongeza,ukiweza nenda pale Sinza mara baada ya kupita Kamanyola ukitokea Shekilango upande wa kushoto,kuna jamaa anauza kuku/kanga na bata Mzinga (kama amehama siku za karibuni sijui),unaweza kuwapata.
Kama ni kwa kufuga,basi jitahidi mkuu,bei yake sokoni hasa wakati wa Noel ni nzuri sana.