mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia Baraza lake la Vijana (BAVICHA), kimeeleza kusikitishwa na hali mbaya ya ajira kwa walimu nchini, kikisema kuwa tatizo hilo ni “bomu linalosubiri kulipuka.”
Akizungumza Februari 15, 2025, wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, Mwenyekiti wa BAVICHA, Wakili Deogratius Mahinyila, alisema kuwa kwa miaka kumi sasa, walimu waliomaliza vyuo hawajawahi kuajiriwa kwa mkupuo, hali ambayo imewaacha wengi mtaani bila ajira.
“Kuna kundi kubwa la wahitimu wa ualimu mtaani, ambao tangu mwaka 2015 hawajapata ajira rasmi. Serikali imekuwa ikiajiri kwa kudonoa donoa tu,” alisema Mahinyila.
Aliongeza kuwa hali hiyo imewakatisha tamaa wazazi, ambao wamekuwa wakitoa sadaka kubwa kusomesha watoto wao kwa matumaini ya maisha bora, lakini mwisho wa siku wanarejea nyumbani bila ajira.
“Wazazi wanatutukana wakisema ‘niliuza ng’ombe kusomesha ng’ombe mwingine, ambaye sasa amerudi hana chochote,’” alieleza Mahinyila, akionyesha hisia za wazazi waliochoshwa na hali hiyo.
Mahinyila alitaja takwimu za serikali za mwaka 2023, zinazoonyesha kuwa bado kuna upungufu mkubwa wa walimu nchini, hasa katika elimu ya awali.
“Uwiano wa walimu wa awali ni mwalimu mmoja kwa watoto 193, wakati inapaswa kuwa mwalimu mmoja kwa watoto 25. Mfano, Mkoa wa Singida mwaka 2023 ulisajili watoto 62,931 wa darasa la awali, lakini kulikuwa na walimu 382 pekee, wakati uhitaji ulikuwa 2,517,” alisema.
Alisisitiza kuwa hata kama walimu wote waliopo mtaani wataajiriwa, bado mahitaji ya walimu nchini yatakuwa makubwa, akitoa wito kwa serikali kuchukua hatua madhubuti kushughulikia tatizo hilo.
Mahinyila alisema kuwa BAVICHA haitakubali kushiriki katika chaguzi ambazo hazilengi kuleta maendeleo kwa wananchi.
“Kama Taifa hili linaendelea kufanya uchaguzi lakini halitatui matatizo kama ajira, maji, barabara, na huduma za afya, kuna haja gani ya kuendelea kuchaguana?” alihoji.
Alisema kuwa vijana wa CHADEMA hawatakubali kushiriki kwenye chaguzi zilizogeuka kuwa “mtambo wa kuua vijana,” akisisitiza kuwa uchaguzi utaruhusiwa tu iwapo serikali itahakikisha kuna ajira, miundombinu bora, na huduma muhimu