Waziri2025
Senior Member
- Sep 2, 2019
- 148
- 379
Baraza la Vijana wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Arusha BAVICHA, limeibuka na kuitaka serikali kuunda tume huru ya uchaguzi kabla ya uchaguzi Mkuu wa Taifa utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Akiongea na vyombo vya habari mapema leo katika ofisi za kanda ya Kaskazini jijini Arusha,Mwenyekiti wa Bavicha Mkoani hapa, Emma Kimambo amesema kuwa suluhisho pekee la kuondoa changamoto na malalamiko katika uchaguzi Mkuu ujao ni kuwa na tume huru ya uchaguzi .
Aidha amesema chadema wamekuwa wahanga wa chaguzi mbalimbali zilizofanyika na wanayo kumbukumbu ya matukio yaliyotokea katika uchaguzi zilizopita ikiwemo wafuasi wao kupigwa,matokeo ya uchaguzi kubadilishwa na masanduku ya kura kuporwa ndani ya kituo cha kura na hiyo imetokana na kutokuwa na tume huru ya uchaguzi .
Amesema Chadema kimejipanga kushika dola na wanauhakika wa kushinda iwapo serikali itakubali kuunda tume huru ya uchaguzi kwa kuwa wanaamini chadema inawafuasi wengi wanayoiunga mkono hapa nchini.
"Chadema tunadai tume huru kwa sababu tumekuwa wahanga wa chaguzi mbalimbali zilizopita kipindi cha nyuma na awamu hii hatutaki yatokee" Amesema Kimambo
Katika hatua nyingine Kimambo amefungua dirisha kwa vijana wa chadema kutumia fursa ya uchaguzi ujao kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ili kuweza kulikomboa Taifa kupitia nafasi za udiwani na Ubunge.
Wakati huo huo Mwenyekiti huyo amesema kuwa Bavicha kinakusudia kufanya ziara na mikutano ya hadhara katika majimbo yote saba ya uchaguzi mkoa wa Arusha lengo likiwa ni kuhamasisha vijana kushiriki kugombea nafasi za ubunge na Udiwani.
Aidha amesema Bavicha imeanzisha utaratibu wa kufanya siasa za kidigitali na kuachana na siasa za makaratasi katika kupashana habari ,ambapo kila mwanachama wa chadema atapaswa kuwa na simu janja inatayomwezesha kupata taarifa za matukio mbalimbali ya chama hicho.
Ends....
Sent using Jamii Forums mobile app