Leo nimetumia tena muda mrefu katika clubhouse ya Bavicha na mada mbili zilikuwa mezani,kesi ya Mbowe na mkutano wa Dodoma.
Mengi yamejadiliwa lakini niweke haya ambayo naamini ni funzo kubwa,
Mengi yamejadiliwa lakini niweke haya ambayo naamini ni funzo kubwa,
- Kuna mchangaji kwa jina la BM ambaye alihoji mawakili wa Chadema kumuita shahidi aliyeugua kichaa.Kuna wakili alimuuliza kuhusu jina la shahidi na Jaji alichoongelea.John Heche aliingilia kati na kuwalaumu moderators kwa kumruhusu huyu lakini Tundu Lissu akatolea ufafanuzi kuwa ni vizuri asikizwe kwani hamuna hoja isiyojibika!!Lissu na Makamu Mwenyekiti na John Heche ni mjumbe wa kamati kuu.Johna Heche alirudi tena kujitetea.Nahisi hapa John Heche alikosa busara.
- Mashambulizi dhidi ya ZZK yalikuwa mengi lakini Abdul Nondo aliingia na kufafanua kwa kina.Nimevutiwa na kauli yake kuwa "jinsi Chadema wanavyoumia kiongozi wao akisemwa vibaya ndivyo ambavyo nao wanaumia kiongozi wao akisemwa vibaya"Naamini somo limeeleweka!
- ZZK alipata nafasi dakika za mwisho lakini tone na kauli yake ilijaa hasira kubwa,alisema "siwezi kumuombea msamaha Mbowe kwani si baba yangu.........Hapa nahisi ZZK hakustahili kuwa ktiaka hali ile.Na hii ilinikumbusha wachambuzi wa mpira waliposema "Mo Dewji anshindwa kutofautisha ni wakati gani yeye ni mwekezaji na ni wakati gani yeye ni shabiki!