Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Kanda ya Victoria limeitaka Serikali kuunda Baraza la Vijana la Taifa litakalojadili masuala ya vijana, kutoa mapendekezo kwa Serikali, na kusaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa BAVICHA Kanda ya Victoria, Fred Michael Masele, alisema kuwa kuanzishwa kwa baraza hilo kutasaidia kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana, hususan tatizo la ukosefu wa ajira.
"Kama mnavyoona, kuna vikundi kama NETO ambavyo vijana wamevianzisha ili kujadili hatima yao ya ajira kwa sababu hakuna jukwaa rasmi la vijana kujadili masuala yao. Ni jukumu la Serikali kuhakikisha kuwa platfomu kama hizi zinakuwepo," alisema Masele.