SI KWELI BAVICHA wametoa taarifa kwa umma kutahadharisha juu ya mipango ovu

SI KWELI BAVICHA wametoa taarifa kwa umma kutahadharisha juu ya mipango ovu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu leo mapema nimekutana na hii barua nimepata mashaka kama imetolewa kweli na BAVICHA tafadhali naomba msaada wa kujua uhalisia wa barua hiyo kwa umma.

IMG_20241021_112846_884.jpg


 
Tunachokijua
BAVICHA ni ufupisho wa Baraza la Vijana CHADEMA, Baraza linalojumuisha vijana wote wa kike na wa kiume ambao ni wanachama wenye umri wa miaka 18 ya kuzaliwa na usiozidi miaka 35.

Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Novemba 2024, BAVICHA kupitia uongozi wake wamekuwa wakihamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la mpiga kura, zoezi lilotamatika Oktoba 20, 2024 ili kupata sifa ya kushiriki katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa na vijiji ni lazima mwananchi awe amejiandikisha katika daftari hilo.

Kumekuwepo na Barua ya taarifa kwa umma inayosambaa mtandaoni na kudaiwa kuwa imetolewa na Baraza la Vijana CHADEMA, ) ikisema baraza la vijana CHADEMA limepokea taarifa kutoka kwa wazee wa chama ya kuwatahadharisha wasitumike katika mipango ovu inayoratibiwa na baadhi ya viongozi wakuu wa chama ya kupanga kuvamia vituo vya uandikishaji na kupora madaftari ya uandikishaji kutoka kwa mawakala.

Je, ni upi uhalisia wa barua hiyo?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa barua hiyo si ya kweli na haijatolewa na Baraza la Vijana CHADEMA kwani haijachapishwa na kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya BAVICHA.

Kadhalika JamiiCheck imebaini mapungufu kadhaa katika barua hiyo yanayothibitisha kuwa barua hiyo haijatolewa na BAVICHA, moja ya mapungufu hayo ni kukosekana kwa sehemu ya chini ambayo huwekwa anwani katika barua rasmi za baraza hilo.

Barua hiyo imehifadhiwa hapa na hapa.
Back
Top Bottom