BAVICHA yawatakia ushindi Serengeti Boys

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) tunapenda kuwatakia ushindi vijana wenzetu wa Timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys watakaoiwakilisha nchi katika mchezo wao wa Jumapili Septemba 18, mwaka huu dhidi ya Vijana wa Timu ya Taifa ya Congo Brazzaville, kuwania kufuzu kushiriki Mashindano ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Timu za Vijana chini ya umri wa miaka 17.

BAVICHA tunapenda kuwatia moyo vijana wenzetu hao na kuwahakikishia kuwa Watanzania wako nyuma yao, wakiamini kuwa kama Serengeti Boys waliweza kuzifunga na kuzitoa nje timu za Shelisheli na Afrika ya Kusini katika hatua hii ya mtoano, kwa idadi kubwa ya magoli, basi wakitambua wajibu wao kwa taifa kupitia michezo, vijana hao wana uwezo wa kuwafunga Congo - Brazzaville hivyo kujihakikishia nafasi ya kuliwakilisha taifa katika mashindano hayo makubwa hivyo kuitangaza na kuipatia heshima nchi yetu.

BAVICHA tunatumia fursa hii kutoa wito na kuwahamasisha vijana wengi nchi nzima kuwatia moyo Serengeti Boys na wale wenye uwezo wa kufika uwanjani kushuhudia mchezo huo, wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yetu hiyo.

Mungu Ibariki Tanzania

Mungu wabariki Serengeti Boys.

Imetolewa leo Septemba 17, 2016 na;

Julius Mwita

Katibu Mkuu wa BAVICHA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…