Bayport yaeleza namna ya kukizi vigezo vya kuomba mkopo

Bayport yaeleza namna ya kukizi vigezo vya kuomba mkopo

Joined
Apr 9, 2022
Posts
66
Reaction score
32
Taasisi ya Kifedha ya Bayport imeeleza namna ya kukidhi vigezo vya kupata Mkopo , pia imesema kwamba hakuna haja yakusafiri muda mrefu au kuandika nyaraka kuomba Mkopo.

Afisa Uendeshaji Mkuu wa Bayport Nderingo Materu amesema kwamba taasisi hiyo inatoa huduma za mikopo kwa watumishi wa umma pekee , ambapo kwa watumishi wa umma pekee,ambapo mikopo hiyo inatolewa kwa njia ya mtandao.

"Bayport imerahisishia mteja kupata Mkopo Kwa njia ya haraka Kwa njia ya mtandao,leo tuna mtambulisha Haji Manara kiwa Balozi wetu kwasababu tafikisha taarifa zetu Kwa wafuasi wengi wanaomfuatilia kwenye mitandao yake ya Kijamii ikiwemo Instagram , Tweeter, na Facebook, "amesema Materu.
IMG-20220822-WA0000.jpg

Wakati huo huo Bayport imempa kandarasi yakua balozi Afisa habari na Mhamasishaji wa klabu ya Wananchi (Young Africans) ambapo matarajio ni kuwa aweze kuitangaza taasisi hiyo kupitia akaunti zake za mitandao ya Kijamii.

Bw.Materu amendelea kufafanua kuwa mteja anaetaka Mkopo anapaswa kupiga simu au kubonyeza *150*49# nakufuata maelekezo .

Kwa upande wake Khaj Manara alisesema kwamba mkataba huo atahakikisha anautendea kutokana na uwezo wake wa ushawishi kupitia mitandao ya Kijamii.

"Masharti ya Bayport siyo mwiba Kwa watumishi wa Umma ambao wanalipwa na serikali pamoja na taasisi zake,hivyo nawasihi wachangamkie fursa hii ,kwani upatikanaji wa mikopo yao ni rahisi sana na inalipwa kupitia simu ya kiganjani popote ulipo." Amesema Manara.

Aidha Khaji Manara alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wachezaji wa mpira wa miguu wenye majina makubwa kutumia mitandao ya Kijamii Kwa ajili ya kujitangaza nakupata kipato kwani baadhi yao wamekuwa wakiachana na soka wanajikuta wanaishi maisha magumu.
 
Naona Bayport mumempa shavu la ubalozi Msemaji wa zamani wa klabu ya simba ndugu Haji Sunday Manara. Hongera nyingi kwake.

Ila niwausie tu watumishi wa Serikali! Kuna benki za kutosha tu nchini. Hivyo msijaribu kamwe kukopa kwenye hizi taasisi za kifedha! Kiukweli riba zao ziko juu sana. Na huwa wanatumia ujanja wa kukupa mkopo ndani ya masaa 24/48! Ila baada ya hapo, cha moto utakiona.

Unaweza kupewa milioni 2, halafu ukaja kulipa milioni 7!! Huu ni wizi na uonevu uliopitiliza! Kama una shida ya mkopo, nenda benki!

Kama hawa Bayport, ndiyo kabisaa! Wamewaumiza sana walimu, manesi, madaktari, polisi, watendaji wa kata, na watumishi wengine wa ngazi za chini! Siku zote hutumia maneno matamu, na yenye ushawishi! Ukiingia tu kwenye 18 zao, umekwisha.
 
Ule utaratibu wakuongeza sifuri waliacha anakufata ofisini unajaza fom mkopo lakitano hao maajent wao na hujiita maafsa

Ukijaza fom anaenda kukaa upya kwake kujaza fom upya harafu inaongezwa sifuri inakua milion 5 harafu unaingiziwa lakitano

Chamoto utakutana kwenye makato pakwenda huna na taarifa zakozote uliatach
 
Naona Bayport mumempa shavu la ubalozi Msemaji wa zamani wa klabu ya simba ndugu Haji Sunday Manara. Hongera nyingi kwake...
Ni kweli mkuu.Hawa jamaa ni siyo waaminifu kabisa.Wanakukopesha 1m Halafu wanakukata 5m.

Ukifuatilia Kwa nini imekuwa hivyo unapigwa danadana hadi utakoma na kujuta kabisa. Na hutachomoa hadi umalize hilo deni lai haramu.
 
Ule utaratibu wakuongeza sifuri waliacha anakufata ofisini unajaza fom mkopo lakitano hao maajent wao na hujiita maafsa

Ukijaza fom anaenda kukaa upya kwake kujaza fom upya harafu inaongezwa sifuri inakua milion 5 harafu unaingiziwa lakitano

Chamoto utakutana kwenye makato pakwenda huna na taarifa zakozote uliatach
K

Ni kweli mkuu.Hawa jamaa ni siyo waaminifu kabisa.Wanakukopesha 1m Halafu wanakukata 5m. Ukifuatilia Kwa nini imekuwa hivyo unapigwa danadana hadi utakoma na kujuta kabisa. Na hutachomoa hadi umalize hilo deni lai haramu.
Wameshajiharibia kitambo! Ni mtumishi wa umma mwenye akili za kiwendawazimu pekee ataacha kwenda benki kama CRDB, NMB, nk. Halafu akaenda kukopa kwenye taasisi yao.

Hawa na Platinum, ni kama mtu na mdogo wake. Wote ni wabambikiaji wa kubwa wa riba kwa wateja wao. Walio waibia wanatosha. Binafsi sifurahii kuona mpaka leo kuna watumishi wanalalamika kubambikiwa madeni ya mkopo na hizi taasisi za kifedha.
 
mnawasaidia watumishi au mnawaibia?!

kama kweli mnalengo la kuwakwamua kiuchumi wakopesheni, Nyumba, vyombo vya moto n.k
 
Hawa mbuzi siwapendi tabia yao ya kunitumia meseji kila wakati... halafu hii mitandao ya simu aisee wanazingua kichizi hivi mnaingiaje ubia na bayport kushawishi watumishi kukopa? Kwanza wanajuaje watumishi hawa jamaaa maana nikiuliza washkaji wengine ambao siyo watumishi wanasema wao hawatumiwi meseji hizo
 
Wameshajiharibia kitambo! Ni mtumishi wa umma mwenye akiki za kiwendawazimu pekee ataacha kwenda benki kama CRDB, NMB, nk. Halafu akaenda kukopa kwenye taasisi yao.

Hawa na Platinum, ni kama mtu na mdogo wake. Wote ni wabambikiaji wa kubwa wa riba kwa wateja wao. Walio waibia wanatosha. Binafsi sifurahii kuona mpaka leo kuna watumishi wanalalamika kubambikiwa madeni ya mkopo na hizi taasisi za kifedha.
Wanaitwa loan sharks kwa kimombo, hizi unaweza kukuta ni taasisi za mafisadi yanayotafuta kutakatisha pesa na hapohapo yakitafuta kuwaibia wanyonge wenye uhitaji kwa kuwarubuni.
 
Msijaribu kukopa Bayport, ni wezi wana lugha chafu ukikopa ukiomba loan balance wanakupiga dana dana, serikali kwa nn hawalioni hili waache kuingia ubiya nao wananyanyasa sana watumishi,
 
Msijaribu kukopa Bayport, ni wezi wana lugha chafu ukikopa ukiomba loan balance wanakupiga dana dana, serikali kwa nn hawalioni hili waache kuingia ubiya nao wananyanyasa sana watumishi,
Naona hawa jamaa wanamkono wa watu wazito waserikali..mana wana namba za watumishi wote nchini na kila siku wanatuma mimeseji yao.

Ewe mtumishi hata kama unashida ya pesa kiasi gani..ogopa sana narudia tena ogopa sana kukopa kwa hawa jamaa..utajuta.

#MaendeleoHayanaChama
 
Bayport wanaumiza sana, juzi nilijaribu kuongea nao kupata mkopo wa mil7 wakanitumia mkataba wao wao unaonesha nitalipa mil19 ndani miaka 8 😃😃😃
Screenshot_2022_1126_193503.png
 

Attachments

  • Screenshot_2022_1126_193503.png
    Screenshot_2022_1126_193503.png
    42.7 KB · Views: 75
Back
Top Bottom