Inasemekana kwamba wakati Jeniffer akiondoka kwenda kushiriki BBA mwaka jana, baba yake hakuwepo nyumbani and he was kept in dark kuanzia kwenye kujaza fomu mpaka alipojulishwa kwamba ameteuliwa kuwa mshiriki wa BBA na hivyo ataiwakilisha Msumbiji. Baba mzazi alikuja kushangaa kumwona binti yuko ndani ya nyumba. Ndipo sekeseke la kutishia kumtaliki mkewe lilipoanza kwamba kwanini mama na binti walimficha hizo habari mpaka anakuja kushitukia anamuona binti yuko ndani ya Jumba?
Baba wa binti kwa kuzingatia heshima aliyo nayo huko kwao (nadhani ni mwana sheria maarufu huko kwao kama kumbukumbu yangu iko sahihi) na pia kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele kupigania haki za akina dada/mama na hasa kuhusiana na biashara za kwenye madanguro, ndipo alipoona kwamba binti yake alikuwa anashusha hadhi ya jina la baba na familia kwa ujumla. Baba akatishia kusambaratisha ndoa (kumtaliki mkewe) kwa tuhuma kwamba mama alishiriki dhambi ya kumruhusu binti aende BBA bila ridhaa ya baba mzazi.
That is why Jennifer alipokuwa anaondoka alisema anatoka for the sake of family na hasa mama yake, impliedly, hakutaka ndoa ya wazazi wake ivunjike kwa sababu ya ushiriki wake kwenye BBA. Kama watu wanakumbuka, siku binti anatoka alipokelewa na baba yake mzazi na kuishia nae kwenda kwao Maputo.
Kurudi kwa binti, inawezekana ni kutokana na ushawishi wake kwamba hatawaangusha wazazi wake kwa ku-misbehave ndani ya jumba na inawezekana pia age-factor. Mzazi ana control ya mtoto aliye under 18, lakini ukishafikisha age ya Jeniifer ya miaka 23 hakuna mzazi anamfunga binti ama kumpangia afanye nini katika maisha yake.
Nilichokiandika ni kile ambacho kilisemwa kwenye forum ya BB ya mwaka jana, na pia magazeti ya udaku kutoka Mozambique.