Elections 2010 BBC juu ya Uchaguzi Tanzania 2010

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2009
Posts
2,874
Reaction score
316
BBC News - Why is there almost no tribalism during Tanzanian elections?

hii ni video inaongelea mambo ya tribalism Tanzania na Uchaguzi. Nimeipenda kweli. Safi sana....

 
Hii ni nzuri sana na imetulia kabisa...huyo kijana ni mfano mzuri kwa vijana wengine ambao ndo kwanza wananza kupiga kura mwaka huu,2010.
 
I can't vote for corrupt regime either!!!!!! Am looking forward to regime change soon after 31/10/2010
 
Jana kwenye taarifa ya habari ya saa 3 usiku (GMT) BBC World News walitufagilia sana Watanzania kwa umoja tulionao. Wanasema inakuwaje nchi yenye makabila zaidi ya 100 wanaishi kwa umoja bila machafuko na hata kwa sasa inaendesha kampeni zake za uchaguzi bila machafuko wala ubaguzi wa kikabila ukilinganisha na majirani zetu. Walionyesha watu wakiwa kwenye kampeni na mgombea peke yake aliyeonyeshwa akinadi sera zake jukwaani ni Halima Mdee huko Kawe. Na hatimaye wakamhoji Prof. Palamagamba Kabudi wa pale kitengo cha sheria UDSM akaelezea chimbuko la umoja wetu. Ilikuwa nzuri sana kwa kweli.
 
jamani 2cishie kuandika vyema ktk mitandao twendeni kuvoti on sunday, asiye voti asitupigie klele kuwa kaonewa, maana hata bible imesema asiyefanya kazi na asile.
 

nina wasi wasi sana kama hali itaendelea kuwa ya kuvumiliana na hivi baada ya tar 31 oktoba 2010 kutokana na maandalizi ya wizi wa kura iliyoandaliwa na ccm pamoja na tume ya uchaguzi. Vijana hawa wemnye matumaini watakata tamaa ya kufanya mabadiliko na sijui nini kitatokea.
 

Yeah,
Tunamwomba sana Kikwete asifanye U-MwaiKibaki. Maana akifanya hivyo anaweza kusababisha machafuko na kuiharibu sifa nzuri ya Tanzania tuliyonayo kwa sasa. MUNGU ni mwema tusiache kuomba ili mipango yote mibaya waliyonayo CCM ishindwe.
Kikwete maisha bila urais yanawezekana. Umeshindwa kuiongoza nchi waachie wengine watuletee maendeleo.
 
mpaka sasa hari siyo nzuri nchini, Kigoma hali siyo kabisa tume wanachelewesha matokeo wkt watu wanajua takwimu kwaani matokeo hubandikwa kwenye vituo vya kupigia kura. hii ni hatari kubwa. CCM walikuwa wanaimba wimbo wa kukubari matokeo sasa mbona wanakataa kusaini matokeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…