Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,926
- 15,634
BBC yaripoti kuwa Urusi imewaua waasi 70 toka Ukraine waliojipenyeza na kuingia kwenye mpaka wa Russia na Ukraine, kwenye mkoa wa Belgorod, wakitumia magarivita ya Marekani ikiwemo MRAPs (Mine-Resistant Ambush Protected vehicles) na Humvees (The High Mobility Multipurpose Wheeled Vehicles).
Wachambuzi wa BBC waeleza kuwa tukio hilo la mpaka wa Urusi kushambuliwa na waasi toka Ukraine kwa kutumia magarivita na silaha za Marekani kunayapa nguvu madai ya Urusi kuwa ilianzisha vita ya Ukraine kwa sababu usalama na uhuru wake (Urusi) vilikuwa vikipangwa kuhujumiwa na magaidi ya Ukraine kwa msaada wa mataifa ya kimagharibi.
Chombo cha habari cha Marekani, The New York Times, kimeyatambua na kuthibitisha kuwa magari yaliyoonekana kuharibiwa au kushikiliwa (mazima) kwenye picha zilizochapishwa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi kwenye tukio hilo la kigaidi ni ya Marekani. Hata hivyo Marekani imejitenga na tukio hilo ikidai kuwa haikusaidia kwa vyovyote ugaidi huo.
Tunaipa pole Marekani kwa kupoteza magari yake ya gharama kizembe kwenye tukio hilo. Hasa magari yake aina ya MRAPs (Mine-Resistant Ambush Protected vehicles) ambapo gari moja bei yake ni kati ya USD 500,000 hadi USD 1,000,000.
====