Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,626
Leo nimekutana na mzee mwenzangu ambaye naye ni BBC (Born before computers), na katika mambo ambayo tumejadili, ni juu ya malezi kwenye familia. Yeye anasema kuwa hawa vijana wa enzi hizi (BAC, born after computers) wana matatizo ya kutojitambua linapokuja suala la mavazi. Aliongea kwa jaziba na kudai kuwa watoto wa kike wamevamia mavazi yetu (ya kiume) na wakome kabisa!!
Nimejaribu kueleza mtazamo wangu kwamba suala la muhimu ni mtu kujitambua na kufanya tathmini ya mahali anapoenda kabla ya kuamua jinsi ya kuvaa.
Huyo BBC mwenzangu kaja juu kabisa....anadai kwamba katika misingi yote (dini n.k) vijana wavae kadri ya maelekezo ya Mungu...Ameahidi kuniletea vifungu kutoka kwenye vitabu vitakatifu vinavyopiga marufuku watu kuvaa nguo za jinsia nyingine.
Tatizo langu ni kwamba....kweli inawezekana kurudi kwenzi hizo za BBC katika mambo ya mavazi?
Naomba michango yenu kabla ya kikao chetu kijacho!!
Babu DC!!