Salaams,
Siku za nyuma kulikuwa na huduma za BBC World Service kwenye baadhi ya maeneo ya Tanzania ambazo zilikuwa zikipatikana moja kwa moja masaa 24 bila kupitia redio station zingine kama Redio one, Tumaini nk. Ilikuwa kama sikosei kwenye FM band 101.4 Mhz.
Kuna mwenye kujua kilichotokea? ...kwa maana haipatikani tena hapo na nimesearch kwenye frequency zote bila mafanikio hivyo kulazimika kukosa habari kama hapo awali.
Naomba mnisaidie wana JF kama ipo kwenye frequency mpya tafadhali.
Nawakilisha