BCom ya UDOM mashaka matupu - Department Haina Majibu

micro_almunia

Senior Member
Joined
Jan 16, 2011
Posts
134
Reaction score
37
Imefahamika kuwa, pamoja na kusajiliwa na TCU, kozi ya BCom inayotolewa na UDOM haitambuliwi na bodi za wataalamu (Professional Bodies kama NBAA, NBMM etc).
Hilo bado halijathibitishwa kwa kozi nyingine ukiacha BCom.
Habari za kuaminika kutoka NBAA zinasema UDOM bado hawakidhi 'vigezo' vya kutambulika japo haikutanabaishwa kwa wazi vigezo ni vipi.
Imeelezwa kuwa NBAA walikuwa na vyuo viwili vinavyoomba kutambulika (UDOM na St.John), lakini ilipitisha uamuzi wa kukitambua St.John na kukikataa UDOM.
Department inayohusika na BCom walipojaribu kuulizwa kuhusu hilo swala walisema, "hawajui". Vilevile, mkuu wa hiyo idara (anayefahamika kwa jina la Anna Njiku) amekuwa mara kadhaa akikata simu za wanafunzi waliomaliza wanaoulizia hilo suala.
Zaidi ya yote, idara hiyo imeelezwa kusambaza taarifa za uongo kwa wanafunzi wa BCom walioko chuoni kuwa tayari wamepata usajili. Mpaka sasa wanafunzi hao wanafikiri mambo yao ni mazuri, huku bodi zikithibitisha tofauti.
Taarifa kutoka NBAA zinaeleza kuwa, wao wanatambua Diploma ya biashara itolewayo na CBE ni bora kuliko BCom itolewayo na UDOM. Watu waliomaliza hiyo Diploma wameruhusiwa kuanzia ngazi ya module C, lakini watu toka UDOM wameambiwa wao ni ngazi ya module B.
SWALI: Je, waajiri wataendelea kuwachukua wahitimu waliokataliwa na professional bodies?
 
Hiyo ni kawaida kwa,chuo kinachoanza ,hakuna chuo kilichoanza na kukubaliwa moja kwa moja kufanya mitihani ya board.
 
chuo kwanza kichanga ktk tahaluma so ni vigumu bodi kuwakubalia kwa mda huu
 
UDOM pambaneni bado mda mnao wa kutosha kutimiza vigezo mtambulike na izo bodi za uhasibu.
 
Asa mbona hzi kampun kama pwc huwa wanaenda kurecruit graduates wa hyo bcom huko udom?
 
Chuo bado kichanga taratibu mtfaika ....
 
Kwanza mtasomaje biashara nyie,businessmen are born naturally,Chagga Oyeee!!!

Sasa watafanyaje biashara wakati NBAA haitambui vyeti vyao. Itabidi wafunge maduka na mabucha ya kitimoto mpaka hapo degree zao za Bcom za UDOM zitakapokuwa acredited.
 
hiki chuo kama kimekaa kisiasa sana, nasikia unakuta mtu ni degree holder amepewa majukumu ya lecturer wakat vyuo vingine lecturer inabidi awe phd holder, mwenye masters anakuwa asst lecturer, degree holders wanakua tutorial asistants huku wakiendelea kusoma.
kitu kingine hapo udom unakuta lecturer mmoja anawanafunzi zaid ya 1500 hebu sema ataweza kumark assignments, tests na mitihan ya hawa watu wote au atakuwa anaguess marks?
 
Wabadilishe mitaala!!!!



NBAA lazima uingize masomo flan, MA, COST, ACC, FM, na mengine mengi
 

Mlete uzi naomba nikusahihishe,siokweli kwamba Bcom ya Udom haitambuliwi na Professional bodies kama ulivyo sema,kwani Bcom ya udom inakozi nyingi yaani b.com marketing,b.com human resorces,b.com intenatinal marketing,bcom small business entrepreneurship,b.com in finance,b.com management sciences,B.COM ACCOUNT etc.

kwa kozi hizo hapo juu ni kozi moja tu ambayo inatatizo unalilo lieleza hapo juu kwa ninavyo jua mimi. so huo mgogoro upo na tatizo ni hao viongozi kwani hawana muda wa kufuatilia hadi wakumbushwe na wanafunzi hasa walio hitimu na ni kweli huyo madam tangu awe mkuu wa idara ndo tatizo limezidi (amewezeshwa).
 

Wewe umeorodhesha maBcom mengi na unasema 1 ndiyo yenye matatizo alaf hauitaji ni ipi kati ya hizo,ni afadhali nimuamini mtoa uzi kuliko wewe maana unatoa habari nusu nusu,na hausemi kwa nini hiyo Bcom.1 ina matatizo.
 
Kifuatacho 'Nimesikitika sana,nimesononeshwa sana,nimegundua tatizo ni Ukuu wa idara nimeamua kujiuzulu naenda Kusoma.Pole dada Anna ila wajibika
 
Wewe umeorodhesha maBcom mengi na unasema 1 ndiyo yenye matatizo alaf hauitaji ni ipi kati ya hizo,ni afadhali nimuamini mtoa uzi kuliko wewe maana unatoa habari nusu nusu,na hausemi kwa nini hiyo Bcom.1 ina matatizo.


B.COM ACCOUNT, peke yake mkuu.
 
Hiyo ni kawaida kwa,chuo kinachoanza ,hakuna chuo kilichoanza na kukubaliwa moja kwa moja kufanya mitihani ya board.

Hoja yako si kweli, chuo kama IAA kilikuwa na graduants wa kwanza mwaka 1999 na mwaka huo wakafanya mitihani ya CPA-T kwa level ya professional level III kwa leo inajulikana kama module E.na wanafunzi walifaulu vizuri kuingia level IV. Kifupi ni kwamba ili waweze kuruhusiwa lazima wawe na wa-lecturers ambao kwa uchache wao wawe recognized by NBAA kama lecturers wao wanakwepa kufanya mitihani ya CPA na kufaulu kazi wanayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…