Wewe umeorodhesha maBcom mengi na unasema 1 ndiyo yenye matatizo alaf hauitaji ni ipi kati ya hizo,ni afadhali nimuamini mtoa uzi kuliko wewe maana unatoa habari nusu nusu,na hausemi kwa nini hiyo Bcom.1 ina matatizo.
Asa mbona hzi kampun kama pwc huwa wanaenda kurecruit graduates wa hyo bcom huko udom?
Imefahamika kuwa, pamoja na kusajiliwa na TCU, kozi ya BCom inayotolewa na UDOM haitambuliwi na bodi za wataalamu (Professional Bodies kama NBAA, NBMM etc).
Hilo bado halijathibitishwa kwa kozi nyingine ukiacha BCom.
Habari za kuaminika kutoka NBAA zinasema UDOM bado hawakidhi 'vigezo' vya kutambulika japo haikutanabaishwa kwa wazi vigezo ni vipi.
Imeelezwa kuwa NBAA walikuwa na vyuo viwili vinavyoomba kutambulika (UDOM na St.John), lakini ilipitisha uamuzi wa kukitambua St.John na kukikataa UDOM.
Department inayohusika na BCom walipojaribu kuulizwa kuhusu hilo swala walisema, "hawajui". Vilevile, mkuu wa hiyo idara (anayefahamika kwa jina la Anna Njiku) amekuwa mara kadhaa akikata simu za wanafunzi waliomaliza wanaoulizia hilo suala.
Zaidi ya yote, idara hiyo imeelezwa kusambaza taarifa za uongo kwa wanafunzi wa BCom walioko chuoni kuwa tayari wamepata usajili. Mpaka sasa wanafunzi hao wanafikiri mambo yao ni mazuri, huku bodi zikithibitisha tofauti.
Taarifa kutoka NBAA zinaeleza kuwa, wao wanatambua Diploma ya biashara itolewayo na CBE ni bora kuliko BCom itolewayo na UDOM. Watu waliomaliza hiyo Diploma wameruhusiwa kuanzia ngazi ya module C, lakini watu toka UDOM wameambiwa wao ni ngazi ya module B.
SWALI: Je, waajiri wataendelea kuwachukua wahitimu waliokataliwa na professional bodies?
mnaniacha hoi na masomo ya biashara!yaani hamtambuliki mpk mpitie nbaa na psptb,wakati geology,education,wildlife,molecular biology,economics,statistics ukimaliza unapeta2.
Ushauri kwa wanaopenda kuajiriwa especially waliosoma pcb,cbg soma livestocks,agric,pharmacy etc. Adv.math e.g egm,pcm,pgm etc.haina haja ya kubanana ktk accounts,procurement.soma b.a statistics au monitoring&evaluation,hautasumbuka sana kupata ajira.usiangalie majina ya kozi.uhasibu,proc. Kila mtu anakimbilia,matokeo yake hadi uje utambulike ufanye mitihani mingiiii!