(Be forward) Bei hizi za magari mitandaoni zipo sahihi kweli?

Nimeagiza Gari tc-v & SBT 1. Usalama wa pesa yako (ukituma pesa Japan, mwenye halipwi mpaka gari iwe shipped) 2. Bei zao nafuu 3. Gari in mint condition
SBT gari zimekula km za kutosha.
 

wanavosema new model kodi yake ni ndogo hawaangalii amount ya kodi ila asilimia ya kodi ukilinganisha na bei ya gari.

lets say rav 4 ya mwaka 1999 bei yake bila kodi ni sh milion 6... alafu kodi yake ni shilingi milion 7 ambayo ni mara mbili ya bei ya gari

ila rav 4 new model tuseme bei yake ni sh milion 60 halafu kodi yake milion 20 (haijafika hata nusu ya bei)

sasa inavo compare usifananisha kodi ya mil 7 ya old model ukafananisha na mil 20 ya new model ukasema new model kodi kubwa bila kuangalia bei zake kabla ya kodi.

Hivyo tunasema new model zina kodi ndogo
 
Mkuu ukiachia kodi ya uchakavu, wapi kuna unafuu?

Import Duty kwa zote ni 25%
Excise duty kwa zote zenye cc chini ya 2000 ni 5% au kama zaidi ni 10%
Vat kwa zote ni 18%

Sasa unafuu huu uko wapi? wamecheza na maneno tu apo, hamna lolote.

Yaani walau wangefanya new models import duty chini ya 25% ndio ningeelewa.
 
Nimependa mawazo mmbadala,tulikuwa tunafikiri kodi kubwa ipo ilivkudhibiti uchakavu lakini si hivyo.Ni bora kodi ikashushwa lakini watu wahamasike kuagiza gari zilizo chini ya miaka 15.

nina maanisha magari ya 2000-2004 leo hii yana miaka karibia 20.Ila kwa sisi ndio tunayagombania.
 
Unaambiwa hata customs processing fees gari new model ipo. Yaani hata processing fee basi pia wameshindwa kuweka chini!

halafu wanawaambia watu kwa maneno kuwa gari mpya kodi ndogo, kodi gani gani hio ndogo? kumbe Uchakavu tu!
 
Kodi inazidi CIF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…