MSALANI;
Venga boys mbona huwataji?
Mkuu, Venga boys (kundi lilianza mwaka 1997) ni watoto wa juzi tu huwezi kuwafananisha na hao waliotajwa. Tukirudi kwenye hayo makundi matatu inategemeana unataka kufananisha nini. Kwa club bangers Boney M (1975) anashinda ingawa kazi kubwa kama kuandika nyimbo na kuzitengeneza ilifanywa na watu wengine, wale kina dada watatu na yule Brotherman walikuwa kazi yao ni kurekodi studio na kufanya shows tu. Halafu Boney M walikuwa na wana-cover sana nyimbo za watu wengine mfano Malaika, Mary's Boy Child (Long time ago in Bethrehem), No Woman No Cry, Rasputin n.k
ABBA (1972) na Bee Gees (1958) kwa wale wanaopenda real music na sio ma-bubble gum wanashinda kwani wao walikuwa ni watunzi wazuri sana wa muziki. Kundi la ABBA kutoka Sweden lilikuwa very interesting kwani liliundwa na two couples yaani jamaa wawili na wake zao (jina ABBA lilitokana herufi za mwanzo za majina yao). Walikuwa wakiandika nyimbo zao wenyewe kisha wanaume wanatengeneza muziki na kina mama wanaimba, na walikuwa na sauti nzuri kweli kweli. Sikiliza nyimbo kama I Have a Dream, Angel's eyes, Fernando, Chiquitita, Take a Chance on Me, S.O.S, Mama Mia n.k.
Bee Gees kutoka Australia (ingawa baadaye walihamia Marekani) liliundwa na ndugu watatu Maurice Gibb (RIP), Bary Gibb na Robin Gibb (RIP). Hawa jamaa walikuwa ni wakali wa melody ile mbaya na walipata umaarufu mkubwa walipotengeneza nyimbo zilizotumika katika sinema maarufu sana ya zamani ya John Travolta iitwayo Saturday Night Fever. Nyimbo zao maarufu ni kama Stayin' Alive, How Deep is Your Love, Saturday Night Fever, Spirits Having Flown n.k.
Sifa yao nyingine kubwa ni kuwaandikia wasanii wengine nyimbo zilizo-hit, mfano Immortality (Celine Dion), Emotion (Destiny's Child), Island in The Stream (Dolly Parton na Kenny Rodgers), I Will Be There (Tina Turner) n.k.
Kwa hiyo unaweza kuona jinsi ilivyo ngumu kulinganisha makundi haya matatu.