Beatles, BeeGees, Abba Group na Boney M nani mkali

vamda

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
895
Reaction score
571
Makundi haya ya muziki yaliutingisha ulimwengu kwa kishndo kikubwa kuanzia katikati ya miaka ya 80 na kushuka chini. Naomba wana JF mnaokumbuka makundi hayo mtoe maoni yenu maana mimi napata utata. Nani 'MKALI' zaidi kati yao.
 
Makundi haya ya muziki yaliutingisha ulimwengu kwa kishndo kikubwa kuanzia katikati ya miaka ya 80 na kushuka chini. Naomba wana JF mnaokumbuka makundi hayo mtoe maoni yenu maana mimi napata utata. Nani 'MKALI' zaidi kati yao.

Venga boys mbona huwataji?
 
Duh ngoja waliokuwepo enzi hizo waje. Mie inaniwia vigumu coz napenda nyimbo hizo na ni janki wa juzi 88. ila napenda ngoma zao.
Ngoja tuwasikia wazee wa zamakale
 
Wanasema inshindwa chagua who is best kama beetles na bon m ,pele na maradona, na sasa messi vs ronaldo
 
Du long time sana,matoz wa kitambo mwageni data na sisi tuwafaham.
 
Makundi haya ya muziki yaliutingisha ulimwengu kwa kishndo kikubwa kuanzia katikati ya miaka ya 80 na kushuka chini. Naomba wana JF mnaokumbuka makundi hayo mtoe maoni yenu maana mimi napata utata. Nani 'MKALI' zaidi kati yao.
Kwa upande wangu nashindwa kuwafananisha hawa ni ngumu kwa sababu tune na style zilikuwa hazifanani kivile ndio maana walivuma kwa wakati mmoja . Ukiwasikiliza ABBA ukimaliza utawasikiliza Bee Gees na hutaboreka kama kweli wewe ni mpenda ngoma.

Ila nakupongeza mdau kwa kunikumbusha makundi haya ,siku Maurice Gibb amefariki nilihisi kama ndio mwisho wa music coz namkubali jamaa mpaka kesho.


 
Last edited by a moderator:
Mh!Wote nawakubali ila kwa club,nadhani Venga boys ndio wako juu zaidi. Uncle John from Jamaica,Brazil,red rose na samba na nyingine nyingi za Venga boyz nazikubali kinoma.
 
MSALANI;
Venga boys mbona huwataji?



Mkuu, Venga boys (kundi lilianza mwaka 1997) ni watoto wa juzi tu huwezi kuwafananisha na hao waliotajwa. Tukirudi kwenye hayo makundi matatu inategemeana unataka kufananisha nini. Kwa club bangers Boney M (1975) anashinda ingawa kazi kubwa kama kuandika nyimbo na kuzitengeneza ilifanywa na watu wengine, wale kina dada watatu na yule Brotherman walikuwa kazi yao ni kurekodi studio na kufanya shows tu. Halafu Boney M walikuwa na wana-cover sana nyimbo za watu wengine mfano Malaika, Mary's Boy Child (Long time ago in Bethrehem), No Woman No Cry, Rasputin n.k

ABBA (1972) na Bee Gees (1958) kwa wale wanaopenda real music na sio ma-bubble gum wanashinda kwani wao walikuwa ni watunzi wazuri sana wa muziki. Kundi la ABBA kutoka Sweden lilikuwa very interesting kwani liliundwa na two couples yaani jamaa wawili na wake zao (jina ABBA lilitokana herufi za mwanzo za majina yao). Walikuwa wakiandika nyimbo zao wenyewe kisha wanaume wanatengeneza muziki na kina mama wanaimba, na walikuwa na sauti nzuri kweli kweli. Sikiliza nyimbo kama I Have a Dream, Angel's eyes, Fernando, Chiquitita, Take a Chance on Me, S.O.S, Mama Mia n.k.

Bee Gees kutoka Australia (ingawa baadaye walihamia Marekani) liliundwa na ndugu watatu Maurice Gibb (RIP), Bary Gibb na Robin Gibb (RIP). Hawa jamaa walikuwa ni wakali wa melody ile mbaya na walipata umaarufu mkubwa walipotengeneza nyimbo zilizotumika katika sinema maarufu sana ya zamani ya John Travolta iitwayo Saturday Night Fever. Nyimbo zao maarufu ni kama Stayin' Alive, How Deep is Your Love, Saturday Night Fever, Spirits Having Flown n.k.

Sifa yao nyingine kubwa ni kuwaandikia wasanii wengine nyimbo zilizo-hit, mfano Immortality (Celine Dion), Emotion (Destiny's Child), Island in The Stream (Dolly Parton na Kenny Rodgers), I Will Be There (Tina Turner) n.k.

Kwa hiyo unaweza kuona jinsi ilivyo ngumu kulinganisha makundi haya matatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…