Mafanikio yanatafutwa popote,katika namna tofauti.Kuna mwingine atafanikiwa hapa nyumbani na mwingine ughaibuni kwani riziki ya mbwa iko miguuni mwake.
Kuhusu suala la kujiunga na jeshi napenda kufafanua kuwa sio 100% kifo kama ambavyo wadau wengi wamekuwa wakiponda,kwani jeshi kama jeshi lina makundi yafuatayo:
Combat list-Hili ni kundi linalojumuisha wapiganaji wa vita hasa na ndio wanakuwa front katika uwanja wa vita wanajulikana kama A echelon,kazi yao ni vita tu wakati wa vita na wakati wa amani wanaweza kusaidia katika majanga (Calamities/Catstrophies).
Kundi la pili ni administration/utawala;kundi hili ni wale wanaowawezesha combatant kukaa na kupigana katika uwanja wa vita.Kazi yao ni kufanya Supply ya chakula,maji,matibabu,silaha,mafuta,matengenezo madogo madogo ya silaha na magari,documentation N.K,KUNDI HILI HUWA MABLI NA UWANJA WA VITA.Na hujulikana kama B echelon.
Kwa taarifa tu ni kuwa kwa Jeshi la US unaweza ku specify kuwa unataja kujiunga na jeshi katika idara fulani hata kama huna ujuzi na hiyo idara na hivyo baada ya mafunzo ya recruit utapelekwa shule ya idara hivyo from the scratch.
Ushauri wangu kwa wadau wanaotaka kutumia nafasi hii please specify vitengo ambavyo hata ukitoka jeshini unaweza kutumia elimu yako uraiani ili utakapotoka Jeshini unaingia mtaani ukiwa na ujuzi na karatasi lako.
Please Don't try to be hero ukaenda special forces,commando,ranger,Delta forces au marines au intelligence.Ukweli utaishia kupata sifa za marehemu na maisha yako yatakuwa jeshi na wewe forever,msilewe sifa na kuwa brain washed,regrets hazitakuwa kwenu binafsi bali hata huku nyumbani ambapo tunasubiri mchango wenu mtakaporudi.
Nasisitiza ujuzi wako wa Jeshi(Combat list)ni aidha hauna au una application ndogo sana ktk maisha nje ya Jeshi.
Nenda kamata fields ambazo zitakufaidisha mtaani kama Medicine,Engineering,IT,Communication,Accounting na Finance na N.K
Mkishapata makaratasi yenu na ujuzi wenu njooni tuutumie hapa nyumbani.Nawatakia kila la kheri mnaofiria kutumia nafasi hii.Inshaallah.