Behind the curtain: September 11

Swali kutoka Whatsapp

Je, Usama aliwahi kuishi nchini Marekani? Na je mafunzo yake ya kivita aliyapata wapi?



JIBU:


Nijibu swali la kwanza kwa uchache tu kwa sababu mwishoni mwa makala nitaongelea masuala yenye utata kuhusu Osama, Marekani na Tukio la 9/11.. Mojawapo ni kama je Osama alikuwa "mshirika" wa Marekani..

Kwa sasa ni jibu tu kama Osama aliwahi kuishi Marekani??


Well, ifahamike kwamba rekodi nyingi sana za Idara ya Uhamiaji ya Marekeni za miaka ya 1970 na kurudi nyuma nyingi hazipo au zimepotea au Kuharibika kwa hiyo ni vigumu kupata taarifa kutoka serikalini kuhusu kama Osama aliwahi kuingia Marekani (au yafaa kusema Serikali ya US inataka watu waamini hivyo)


Lakini uko ushahidi unaoonyesha kwamba miezi michache kabla ya Urusi kuivamia Afghanistan Osama bin Laden alitembelea Marekani..


Ushahidi hii unaungwa mkono na mke wa kwanza wa Osama anayeitwa Najwa bin Laden pamoja na rafiki wa Osama wa ujanani anayeitwa Khaled Bartarf..
Wote wanasema kuwa wanakumbuka hii ilokuwa ni mwaka 1979.


Katika kitabu cha Najwa kinachoitwa "The Bin Ladens: An Arabian Family in the American Century", kuna kurasa Najwa anaeleza kuwa, kuna siku Osama alirudi Nyumbani usiku na kumueleza wajiandae wanasafiri kwenda Marekani siku chache zijazo.

Najwa anasema alishangaa safari hii ya ghafla kwani Osama alikuwa na desturi ya kushauriana naye kuhusu mambo yahusuyo familia yao, lakini kutokana na mila za Kiarabu hakuhoji chochote kuhusu safari hii.


Najwa anaeleza kuwa katika safari yao hii walipitia London na baadae wakaelekea Marekani maeneo ya Indiana.

Wakiwa Indiana mtoto wao mmoja aliyeitwa Abdul Rahman akaapata homa kali, na hivyo wakampeleka hospitali.
Najwa anaeleza kuwa hii ilikuwa ni moja kati ya mara yake ya kwanza kuwa karibu kiasi hicho na wazungu, ambapo ni daktari aliyekuwa anamtibia mtoto wake Abdul Rahman.


Najwa anadai kuwa daktari na manesi walikuwa ni wapole kwake na wakarimu mno na hii ilimfanya abadili mtazamo wake juu ya wazungu tofauti na alivyokuwa anaamini.

Najwa anaeleza kuwa siku chache baadae Osama aliwaacha Indiana na yeye akaelekea Los Angels ambako inaaminika kuwa alienda kukutana na 'mentor' wake Abdullah Azzam ambaye alikuwa Marekani kipindi hiki. (Ikimbukwe kuwa kilindi hiki Marekani waliunga mkono waislamu wenye msimamo mkali wa Mujahedeen, miaka ya baadae hata MAK (Muktab al-khidamt) walifungua ofisi Marekani).


Najwa anaeleza kuwa walipokuwa wanarejea Saudi kuna mahala walikuwa kwenye uwanja wa ndege wa Marekani na alikuwa amevalia Abaya jeusi na Hijab.. Anaeleza kwamba wazungu walimshangaa sana na wengine wakaanza kumpiga picha.


Rafiki wa Osama wa kipindi hiki cha ujana Bw. Khaled Bartarf anaeleza kuwa Osama aliliongelea sana tukio hili alipotudi Saudi, na aliliongea sio kwa kuchukia au kuudhika bali aliongea kwa utani.! Khaled anakumbuka Osama alikuwa anasema kwa utani kuwa "it was like being in a show" (kwa kiarabu).


Hii ni moja ya visa vilivyothibitika kuwa Osama aliwahi kuingia Marekani.


The Bold
 
nimesema google 911 truth au 911 inside job utapa habari za kukutosha kujiridhisha kwamba 911 ni inside job. Unahitaji msaada gani tena?
Credibility ya source na story yenyewe navyo vina matter sana otherwise inabaki kuwa concipiracy theory tu kuwa ni inside job.
 
Lkn mkuu hilo la mjapani aliekufa kwenye ndege lipo kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Hakuwa pilot kama anavyotuhadithia the bold, labda hii hadithi ya the bold iwe anatunga yeye mwwnyewe.
Ndugu yangu ngoja nikueleweshe vizuri watu wengi tumekuwa tukiamini katika vitu viwili kuwa ndio chanzo pekee ya habari au taarifa tumekua tukiamini GOOGLE ndio maana kila kitu mtu anakimbilia Google bt tumeshindwa kujua Google ni search engine tu

Pili tumekuwa tukiamini WIKIPEDIA kama ndio sehemu ya kuverify taarifa au habari bt nataka kukwambia Wikipedia wanatoa taarifa kwenye site mbalimbali ndio maana kwa chini kabisa wanatoa References ya sehemu walipotoa taarifa zao wikipedia wamekuwa wakichukua taarifa zao nying kwenye vyombo au site za West
ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kupotosha habari au kupendelea ktk kutoa habari

Mfano ukiangalia ktk vita vya israel six days war June 5–10, 1967 hakuna sehemu yeyote waliosema juu ya mchago wa US,UK na France kwa Israel juu ya vita vile lakini walichangia sana juu ya vile vita hii imepelekea watu kuamini kuwa Israel ilipigana peke yake lakini kama ukitafuta hv vitu vinaelezea ukweli juu ya ushiriki wa nchi hzo nilizotaja

Kitabu cha General Steven Green wa US Army kitabu kinaitwa (The Six days war cha mwaka 1981)

Tafuta Gazeti la New York Times la Sep 21,1995

Tafuta video ya kikao cha UN cha Sep 1 ,1969

Tafuta mdaharo wa Wagombea urais wa US mwaka 1993

Vyote vinavyo ninaweza kukutumia popote duniani kama utaitaji so vyote vimeelezea vizuri ushiriki wa nchi za magharibi na US ktk vita vile upande wa ISRAEL lakini ukienda wikipedia huwezi kuta taarifa hzo


Sasa bhasi kuhusu kushiriki kwa Khalid Shaikh Mohammed(KSM) katika kile kijulikanacho kama Bojinka plot nchini Philippine alichoelezea The bold ndio sawa kabisa kuelewa vizuri Tafuta kitabu cha The History of 9/11 kilichotoka mwaka 2005 kilichoandikwa na Amrullah Saleh aliyekuwa anafanya kazi Inter-Services Intelligence na CIA na yeye ndie aliyefanikisha kukamatwa kwa huyu KSM March 1, 2003 Rawalpindi , Pakistan

Bwana Amrullah ndie aliyepewa kazi ya kumfatilia KSM toka mwaka 1987 alipokwenda nchini Afghanistan so amekuwa akifatiliwa na huyu bwana Amrullah anamjua vizuri sana KSM

So ktk kitabu hicho ukurasa wa 102 bwana Amrullah anaelezea KSM na safari yake ya nchini Philippines mwaka 1991 ninamnukuu

" Khalid Shaikh Mohammed (KSM) first “earned his spurs” in al-Qaeda by serving as one of Osama bin Laden’s first bodyguards. Then, in 1991, bin Laden sends KSM to the Philippines where he trains members of the militant groups Abu Sayyaf and the Moro Islamic Liberation Front (MILF) in bomb making and assassination. He works with bin Laden’s brother-in-law Mohammed Jamal Khalifa to establish an operational base there and also in Malaysia.

Nadhani kwa kauli hyo unaweza kujua kuhusika kwa bwana Khalid Shaikh Mohammed (KSM) ktk tukio la Bojinka plot

Ktk ukurasa wa 105 anaelezea namnukuu

" he also works with his nephew Ramzi Yousef, who trains Abu Sayyaf militants the same year (see December 1991-May 1992). “After proving himself an outstanding organizer, [KSM] was given substantial operational authority and autonomy by bin Laden.”

Huyo bwana RAMZI YOUSEF ambayo hiyo Wikipedia ndo inamtambua kama mfanya tukio la Bojinka plot

Mm najua kwa nini bwana KSM amewekwa hapa lakini nataka kukwambia The bold mpka sasa yuko vizuri hakuna kitu alichotunga hapa nafatilia kwa ukaribu story hii na pia The bold source zake ni zakuaminika na makini najua hicho ndio maana nakwambia hvyo so kuwa na amani tuenjoy story
 
Kwa hiyo unakubaliana na the bold kwamba mjapani aliekufa kwenye jaribio la bojinka plot alikuwa ni pilot?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…