Kig
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 1,076
- 458
Jamani kuna pagale (nyumba ambayo haijapauliwa) maeneo ya mtwivila, nje tu ya geti la chuo cha mkwawa iringa linauzwa. Limejengwa kwa tofali za kuchomwa, lina linta imara kabisa, kuta zote zimeisha, lina bedrooms 4, sebule 1 na jiko 1, shimo la choo limejengwa tayari, pia kuna eneo la kujenga parking. Chumba kimojawapo kinaweza kutumika kama frem ya biashara maana dirisha lake lipo upande wa barabarani. Bomba la maji limepita mita 5 toka kwenye nyumba, umeme upo jirani kabisa wala huhitaji nguzo ya umeme ili kuingiza umeme ndani ya nyumba, barabara ipo na nyumba inafikika kwa gari ya aina yoyote hadi uwanjani. Bei ni million 10 tu. Lakini Maelewano yapo pia. Unaweza uni PM kwa maelezo maongezi zaidi