Bei Kandamizi: Waziri Kalemani azuia gharama za umeme za Sh. 2,000 hadi 3,700 badala ya Sh.100 kwa unit moja

Bei Kandamizi: Waziri Kalemani azuia gharama za umeme za Sh. 2,000 hadi 3,700 badala ya Sh.100 kwa unit moja

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Waziri wa Nishati, Dkt. Kalemani amefanya ziara kisiwa cha Maisome Mwanza na kuagiza kampuni binafsi inayosambaza Umeme katika kisiwa hicho kutoza bei elekezi ya Serikali ya Umeme Vijijini ya Tsh 100 kwa unit moja badala ya Tsh 2,000/- mpaka 3,700/- iliyokuwa ikitozwa.

My Take:
Inaonekana kama Serikali ilikuwa haijui hizi bei zinatozwa huku. Je Serikali ilikuwa haijui?

Tujiulize hii Kampuni ilikuwa hailipi kodi kutokana na hayo malipo?

Serikali haikubariki hizi bei kwa kupokea kodi inayotokana na malipo makubwa?, Na kama Haikubariki imeichukulia hatua gani hii kampuni maana kutakuwa na ukwepaji kodi hapo au kukiukwa kwa masharti ya mkataba?
 
Hivi hakuna chombo cha kusimamia bei?

Kama kipo kinafanya kazi gani? Yaani Waziri yeye akihamua ameshahamua.

Mhe. Rais angalia mienendo ya Mawaziri wako.
 
Waziri wa Nishati, Dkt. Kalemani amefanya ziara kisiwa cha Maisome Mwanza na kuagiza kampuni binafsi inayosambaza Umeme katika kisiwa hicho kutoza bei elekezi ya Serikali ya Umeme Vijijini ya Tsh 100 kwa unit moja badala ya Tsh 2,000/- mpaka 3,700/- iliyokuwa ikitozwa...
Hiyo kampuni iliuwa na dikteta now hayupo watu wamemgeuka
 
Ni wapi serikali yetu kupitia TANESCO wanauza umeme 100 kwa unit moja?

Mbona ni 390/-!
 
Back
Top Bottom