Hawa jamaa wa TTCL sio wakweli kuwa gharama yao ni T.SHS 45,000 kwa mwezi kwani hawana kadi za shs. 5,000 kwahiyo unapokwenda kulipia wanakwambia utoe shs.50,000 kwani hawana kadi za shs 5,000!! Huu ni utapeli wa mchana kweupe. Kama walijua hawana kadi za shs 5,000 kwanini waliweka bei isiyoendana na kadi wanazouza? Kuna umuhimu wa hawa jamaa kurekebisha kasoro hii ama sivyo waseme tu kuwa charge yao ni SHS.50,000 kwa mwezi.