Bei ya dagaa mkoa wa Mwanza iko juu kuliko mikoa mingine kwa ajili ya kupima kwa kutumia vitini/visado

Bei ya dagaa mkoa wa Mwanza iko juu kuliko mikoa mingine kwa ajili ya kupima kwa kutumia vitini/visado

ndege joni

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
682
Reaction score
1,108
Habari zenu wote, na poleni na changamoto za maisha zikiwemo maradhi.

Kwa utafiti wangu usio rasmi nilioufanya, nimebaini bei ya dagaa wa Mwanza katika mkoa wanakotoka iko juu kuliko mikoa mingine Tanzania kwa sababu ya matumizi ya makopo maarufu kama vitini/visado.

Baadhi ya mikoa ikiwemo Morogoro, Arusha, Dodoma na Singida wanaopima kwa kilo, bei ya kilo 1 iko kati ya 5000 na 6000 kwa dagaa wa Mwanza na kati ya Tsh 6000 na 7000 kwa dagaa wa Bukoba.

Nimejaribu kununua dagaa wa Mwanza kwa zaidi ya wauzaji watano tofauti wanaouza kwa bei ya kati ya 4500 na 6000 kwa kitini kwa dagaa wa Mwanza na kati ya Tsh 6000 na 7000 dagaa wa bukoba kwa kitini na kubaini kutokana na upimaji wao kitini kimoja kina ujazo wa kati ya gramu 450 mpaka 700 ambazo ni wastani wa nusu kilo.

Kwa mantiki hiyo dagaa wa Mwanza wanaofaidi sio wazawa bali ni Mikoa mingine.

Nadhani kwa hali hii kuna haja ya waziri mwenye dhamana kupiga marufuku matumizi ya makopo/visado/vitini kwa maslahi ya wananchi.

Hata ukifatilia utagundua wafanya biashara wa dagaa mkoa wa Mwanza ni matajiri sana kutokanana na utapeli wanaoufanya.
Naleta hoja mezani.
 
Dagaa unanunulia wapi? Itakuwa wakujaa kule kwetu ukereweee dagaa ni mbogaa ya chini Sanaa, Kuna wanguzi nenda mwaloni! Kuna walanguzi Ila dagaa ni bei poa.

Njoo Mswaili uonee bei ya dagaa,Ila pia chambua dagaa wakavu wa maweee(wasio na mchanga)au dagaa wakavu wanao anikwa kwenye mchanga au dagaa wa kukaanga
 
Back
Top Bottom