Bei ya dhahabu sasa yavuka $ 1,100 - Kikwete anakwenda jamaika kutafuta ....?


Ubahiri mzuri ni tofauti na kuwa mchumi mzuri.
 
alicho fanya Mkapa na wenzake ni wizi mtupu, sio kwamba walikuwa hawajui ku-sign mikataba yenye maana kwa taifa bali wali weka maslahi yao mbele/wizi, kwa kutumia ujinga wa Watanzania Wengi ambao wamewanyima elimu, umeme, barabara nk ilikuendeleza ujinga wao na wao wawe ndio wafalme wa njii hii.
na hata sasa hivi kikwete hataki kuimplement report yake ya bomani, ilikuendeleza wizi huo na kuwadumaza wa tanzania. kwa kweli matusi wanayo watukana atanzania ni makubwa mno. wanastahili kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi.
 
...... vasco da gama yeye anataka kwenda jamaica.

Si alishatueleza kuwa safari zake za nje ni kwa ajili ya faida ya nchi? Kama vile kutafuta wawekezaji nk.? Labda Jamaica wana some sort of a "reggae scheme" wataintroduce Bongo.

😀
 
Zakumi,

waweza kusema kuwa makonsavativu wengi ni mabahiri?


Conservatives wako wa aina mbili hivi. Kuna wale fiscal conservatives ambao wanataka serikali kuwa na balance budget, kuachia huduma muhimu kufanywa na private sector.

Na kuna social conservatives ambao wanataka sheria za nchi au jamii zifuate misingi ya dini au utamaduni.

Hivyo kama mzee mzima alikuwa conservative basi nitamweka kwenye kundi la pili. Kwa sababu hakuona matatizo yoyote yale ya Ujima.
 
Wenzetu Zambia wamefuta mikataba yote na sasa sheria ndiyo inayotumika. Nilipata kuzungumza na Mkurugenzi wa Madini, Mkurugenzi wa Usalama wa Migodi pamoja na Mhandisi Mkuu na wote walisema walikuwa wanaibiwa na kama kampuni hizo zinataka kwenda mahakamani ziende. Mpaka sasa kampuni karibu zote zimeufyata isipokuwa moja ambayo nayo kesi yake ni dhaifu sana. Lakini serikali yetu inasema mkataba hiyo batili ni mitakatifu. Utakatifu unaozungumziwa ni rushwa ambayo wale waliokula na wanaoendelea kula wanajua wataikosa. Mambo haya yanatia uchungu na ndiyo maana tumelazimika kwenda mahakamani kudai haki.
 
Zakumi,
I wouldn't put Nyerere in the conservative category. Politically he was a progressive or even radical. He believed in the total liberation of the black man in the context of the colonization and exploitation that Africa went through.
 
Zakumi,
I wouldn't put Nyerere in the conservative category. Politically he was a progressive or even radical. He believed in the total liberation of the black man in the context of the colonization and exploitation that Africa went through.

Kwa hiyo hatuwezi kusema Nyerere alikuwa conservative kwa kutotumia dhahabu kama watu wanavyotaka kusema hapa.

Kwa kipindi kile wachimbaji wengi walikuwa na hisa katika machimbo yaliopo Afrika Kusini ambayo ilikuwa chini ya ubaguzi. Kwa mfano kulikuwepo tayari machimbo ya dhahabu Geita toka enzi ya mkoloni. Lakini kutokana na uhusiano wa kampuni hiyo na kampuni za South Afrika, migodi hiyo ilifungwa. Na alistisha biashara ya kampuni nyingi zilizokuwa na uhusiano na Afrika kusini.

Sababu nyingine hakupata fair deal kwa sababu kipindi cha utawala wake, biashara ya migodi ilikuwa ni capital intensive. Lakini maendeleo ya kitechnologia na movement za capital zimebadilisha investments katika sekta za madini.

Kwa kumalizia tu. Kusema kuwa Nyerere aliachia dhahabu vizazi vijavyo hakuna maana yoyote kiuchumi na kwenye maendeleo ya jamii. Gold is not a renewable resource, hivyo ingefanya kazi nzuri sana kipindi kile population ya Tanzania ilipokuwa ndogo.
 
Meanwhile.....



http://online.wsj.com/article/SB125979439530273643.html?mod=wsj_share_facebook
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…