Bei ya gesi imeshindikana kushuka au EWURA hawana meno?

Bei ya gesi imeshindikana kushuka au EWURA hawana meno?

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau!

Wiki iliyopita kuna taarifa kuwa bei za gesi za majumbani (LPG) zimepanda watu wakalalamika sana mpaka Ewura wakatoa tamko.

Lakini cha ajabu bei haijashuka bado imepanda mtungi wa 6Kg tuliokuwa tunanunua 18,000/= kwa sasa 20,000/= maisha yamekuwa magumu sana maaana hata mafuta ya kupikia nayo yamefikia 5000/= kwa lita mamlaka husika hazina maajabu?🤔🤔🤔
 
Watu wa Dar bwana mbona sisi mikoani hizo bei tunazo kitambo ,huwa Kati ya 20,000- 22,000
Kwa hiyo unajisifia kununua kitu bei ghari hapo Zambia umeme upo chini kweli biashara ya gesi haiwezi kufanya vizuri maana kutumia jiko la umeme bill yaje kwa mwezi sio kubwa...hapa tunahangaika na mitungi gesi ikiisha umeme upo ila bado mtu ataumiza kichwa kupambana gesi ipatikane ingawaje nayo ipo bei juu..
 
Haya mambo ni kuleta siasa tu kupiga blah blah blah siku zipite...

Tungepata breakdown ya cost of production, wakala anapata ngapi na kodi ni kiasi gani tungejua tatizo lipo wapi...
 
Hizi tozo alizoziasisi madelu umeanza kuwa ndo utaratibu wa maisha, gesi haitakiwi kupanda bei hata kwa bahati mbaya bali serikali makini inatakiwa hata kwa kuweka ruzuku au kuondoa kodi gesi ipatikane kwa bei nafuu zaidi................mtaigeuza hii nchi jangwa kwa kuendekeza ungese....
 
Utakuwa unaishi ushuani sana ww
Ushiani hawauziwi kwa Bei ya juu.
Supermarkets Zina Bei za chini sana.
Wanaoumia na kupanda Bei kwa vitu hii awamu Ni sisi wa Kigogo, Mburahati, Temeke, Buza na Gongo la mboto.
Washua tozo haziwahusu wao Ni benki transfer.
Kupanda mafuta hakuwahusu wao wanamagari ya serikali au ya mashirika.
 
Back
Top Bottom