BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Na Bwanku M Bwanku
Kagera ni moja ya mkoa wa kilimo na mazao mbalimbali yanalimwa. Kwasasa ni msimu wa zao la kahawa ambalo ni moja ya zao linalolimwa.
Toka Tanzania ianze, bei ya zao la kahawa ilikua inagotea kuishia 1,100 kuzunguka hapo lakini leo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan bei ya kahawa imepanda kwa karibu mara 4 kwa mpigo. Wakulima walioanza kuuza kahawa katika Vyama vya Msingi (AMCOS) kwenye Wilaya ya Karagwe wameuza Tsh 4,100 kwa kilo kwenye mnada uliofanyika Juni 5.
Moja ya Mkulima wa kahawa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa amekiri kupanda maradufu kwa bei ya kahawa.
Waziri Bashungwa anasema Juni 5, 2024 amepeleka kahawa yake kwenye Chama cha msingi Bweranyange wilayani Karagwe kuuza ambapo anatoa ushuhuda kwamba kilo ya kahawa aina ya Arabika kwa mnada wa leo Juni 5 ameuza kwa Tsh. 4,100 kwa kilo ya maganda ya Arabika.
Mhe. Bashungwa anasema wakulima wa Kagera hii ni shangwe tupu na haijapata kutokea. Kwa miaka mingi kahawa iligota kwenye Tsh. 1,100 kwa kilo hadi Mhe. Rais Samia alipoingia madarakani na kuingilia kati kuhusu kuzorota kwa bei ya kahawa kwa muda mrefu.
Waziri amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sera nzuri za kuinua zao la kahawa pamoja na Wizara ya Kilimo chini ya Waziri wake Hussein Bashe na timu yao kwa kusimamia vyema bei na sasa wakulima mkoani Kagera wananufaika zaidi.
Na Bwanku M Bwanku.