Bei ya kahawa Tanzania

Mujwahuzia

Senior Member
Joined
Nov 17, 2011
Posts
137
Reaction score
31
Wana jukwaa ninasikitishwa sana na bei ya kahawa nchini kwetu ukilinganisha na wenzetu wa Uganda ukizingatia kwamba wao ni lazima waipitishe nchini kwetu kkabla ya kwenda kwenye soko la dunia. sasa iweje wao bei juu kuliko hapa kwetu
 
Magamba wanakula percent. Mmeshauzwa! Acheni kuilimi ili wele mchanga maana wamezidi.
 
Mkuu naomba utufahamishe tofauti yake kibei zaidi ni ngapi? Ninahitaji kahawa aina ya arabica kuanzia tani moja kila mwezi.
 
Mbona bei poa tu, Kahawa tungu kikombe Sh 100 ukiwa na 200 unapata na kashata ... oh .... Okay, you mean the crop? Why, Arusha farmers have been uprooting theirs opting for maize, beans etc
 
Wana jukwaa ninasikitishwa sana na bei ya kahawa nchini kwetu ukilinganisha na wenzetu wa Uganda ukizingatia kwamba wao ni lazima waipitishe nchini kwetu kkabla ya kwenda kwenye soko la dunia. sasa iweje wao bei juu kuliko hapa kwetu

Mkuu weka data na grade ya hizo kahawa na sisi tujiridhishe.
 
MKUU suala la KAHAWA ni kichefuchefu. Kama lilivyo suala la Korosho na mazao mengi ya kilimo kwa Tz. Nadhani wakulima wa Mbinga (Mbeya/SOngea) na Kalinzi (kigoma) wamejaribu kuvuka vikwazo! Kahawa uganda hununuliwa Tanzania kwa bei nzuri, na wao huisafirisha kwa njia za magendo kwa GHARAMA kubwa hadi nchi mwao! Mi nijuavyo kodi (rasimi na zisizo rasimi) kwa mazao ya kilimo ni nyingi sana na kimsingi inakatisha tamaa wafanya biashara wazalengo na kuondoa uwezekano wa kuwa na SMEs ambazo zingekuwa na kuwa makampuni makubwa ya ku-export!
 
Kwema wadau?
Kahawa inaanza kuvunwa miezi IPI kwa Tanzania?
Wazoefu Tafadhali.....
 
Mkuu naomba utufahamishe tofauti yake kibei zaidi ni ngapi? Ninahitaji kahawa aina ya arabica kuanzia tani moja kila mwezi.
Nenda ,Mbinga (Ruvuma) au kagera , na Iringa (Mfindi ) kuna mzalishaji anaitwa MTC. Pia inapatikana Mbozi(Mbeya)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…