Mzee wa Code
Member
- Sep 23, 2024
- 61
- 91
Akijibu swali la Mbunge wa Korogwe, Timotheo Mzava, Naibu Waziri Judith Kapinga alisisitiza kuwa bei ya umeme kwa mijini kuunganishwa ni shilingi 320,000 na vijijini kupitia miradi ya REA ni shilingi 27,000.
Pamoja na majibu hayo, jambo hili liliendelea kuwa mjadala wakati wa uchangiaji jioni ambapo Mbunge wa Iramba Mashariki, Francis Isack Mtinga, alitoa mfano wa kijiji kilichopo jimboni kwake alichokitajia kwa jina la Iguguno, akisema kuwa kinachajiwa gharama za kuunganisha umeme shilingi laki tatu na ishirini. Mtinga alihoji kwanini bei hii inaendelea kuchajiwa na Tanesco katika maeneo ambayo sio sahihi kama Iguguno, maana ni kijijini.
“Jambo hili tumeshasema hapa mara nyingi, lakini Tanesco wamekuwa wagumu sana kutekeleza jambo hili. Kila wakati ukiwafuata wanasema michakato inaendelea nchini nzima,” alisisitiza Mtinga.
Aliongeza kuwa bei ya kuunganisha umeme kuendelea kuwa hiyo inafubaza maendeleo ya Watanzania, na akapendekeza bei ya umeme iwe shilingi ishirini na saba hata mijini, kwa sababu miundombinu ya mjini ni rahisi.