Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Bei ya mafuta imeendelea kupanda katika masoko ya barani Asia baada ya mkutano wa nchi zinazosafirisha mafuta kwa wingi duniani OPEC kuvunjika bila makubaliano juu ya mpango ulionuiwa kuongeza uzalishaji.
Kuvunjika kwa mazungumzo kati ya mataifa wanachama wa OPEC na wadau wengine kumeongeza uwezekano wa mafuta kufikia bei ya dola 100 kwa pipa, kiwango ambacho hakijawahi kuonekana tangu mwaka 2014.
Hali hii imeibua hofu kuhusu mfumuko wa bei, ambao yumkini ukazilamisha benki kuu kubadili sera zao za kufanya miamala ya fedha au kuongeza viwango vya riba mapema kuliko ilivyokuwa imepangwa hapo kabla.
Masoko ya hisa barani Asia yameonekana yakiyumba huku likizo fupi ya siku ya uhuru ya Marekani siku ya Jumatatu ikiwa na maana hakukuwa na vichocheo vingi vya ununuzi wa hisa. Masoko ya hisa ya Tokyo, Singapore, Seoul, Mumbai, Bangkok na Jakarta yote yameshuhudia thamani ikipanda, lakini masoko ya Shanghai, Sydney, Wellington, Taipei na Manila yameporomoka. Thamani ya hisa katika masoko ya hisa ya London, Paris na Frankfurt iliporomoka muda mfupi baada ya kufunguliwa kwa ajili ya biasahra.
Makampuni ya teknolojia katika kisiwa cha Hong Kong yamebaki katika hali ya wasiwasi kutokana na hofu ya ukandamizaji mpya kwa sekta hiyo na maafisa wa China ambao utazifanya hisa zisiwavutie wawekezaji.
Nchi wanachama wa OPEC na wadau wengine walifuta mkutano wao siku ya Jumatatu ulionuiwa kutafutia ufumbuzi mkwamo kati ya Falme za Kiarabu na wanachama wengine kuhusu jinsi ya kuongeza utoaji na usafirishaji mafuta. Hakuna tarehe mpya ya mkutano iliyotangazwa.