Wapendwa humu JF bila shaka mtakubaliana nami kwamba kwa miezi kadhaa bei ya mafuta ya petroli na dizel imeendelea kupaa tu hapa Tanzania. Kwa baadhi ya maeneo bei imefika hadi 2,700-2,800 kwa lita moja.
Natamani kujua sababu ya bei kwenda juu kiasi hicho, na upandaji huo kuendelea bila kubadilika kwa kushuka.
Kwa kuzingatia umuhimu wa bidhaa hiyo, pia serikali kupitia mamlaka husika ingeliangalia hili suala, kulitolea ufafanuzi na pia kuangalia namna ya kudhibiti bei isiendelee kupaa.
Maisha yamekuwa magumu sana yaani sana, kwani mafuta yanagusa kila mahali na yanagusa maisha ya kila mtu😭😭😭😭😭