Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imepunguza bei ya mafuta kwa mara nyingine katika kipindi cha miezi mitatu huku punguzo la sasa likitajwa kuwa ni la chini zaidi katika kipindi cha miaka sita.
Punguzo la chini zaidi la mafuta liliwahi kutokea mwaka 2009 ambapo bei ya Petroli ilishuka kutoka Sh2,200 hadi Sh1,147.
Jana Ewura ilitangaza kushuka kwa bei za mafuta ambayo kuanzia leo petrol itauzwa Sh1,652, dizeli Sh1,563 na mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh1,523 kwa Dar es Salaam.
Hata hivyo, mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo jana aliiambia Mwananchi kuwa kushuka huko kwa bei ya mafuta si kwa kutisha kwani ni kawaida kwa nishati hiyo kupanda na kushuka kwa kasi.
"Hii ni mara ya pili kwa bei ya mafuta kushuka kwa kiasi hiki hadi kufikia Sh1,652. Iliwahi kutokea Mei mwaka 2009, na ikapanda tena kwa kasi hadi kufikia Sh2,000 na zaidi. Baada ya hapo haikuwahi kushuka," alisema. Hata hivyo, Kaguo alisema kwa kipindi kile viwango vya kubadilisha fedha vilikuwa ni tofauti, akitoa mfano wa mwaka 2009 kuwa Dola moja ilikuwa chini ya Sh1,000 lakini kwa sasa ni zaidi ya Sh1,800." chanzo.http://www.mwananchi.co.tz/habari/K...-tena/-/1597296/2642158/-/3b90tl/-/index.html