Bei ya Petroli yashuka tena

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imepunguza bei ya mafuta kwa mara nyingine katika kipindi cha miezi mitatu huku punguzo la sasa likitajwa kuwa ni la chini zaidi katika kipindi cha miaka sita.

Punguzo la chini zaidi la mafuta liliwahi kutokea mwaka 2009 ambapo bei ya Petroli ilishuka kutoka Sh2,200 hadi Sh1,147.

Jana Ewura ilitangaza kushuka kwa bei za mafuta ambayo kuanzia leo petrol itauzwa Sh1,652, dizeli Sh1,563 na mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh1,523 kwa Dar es Salaam.

Hata hivyo, mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo jana aliiambia Mwananchi kuwa kushuka huko kwa bei ya mafuta si kwa kutisha kwani ni kawaida kwa nishati hiyo kupanda na kushuka kwa kasi.

"Hii ni mara ya pili kwa bei ya mafuta kushuka kwa kiasi hiki hadi kufikia Sh1,652. Iliwahi kutokea Mei mwaka 2009, na ikapanda tena kwa kasi hadi kufikia Sh2,000 na zaidi. Baada ya hapo haikuwahi kushuka," alisema. Hata hivyo, Kaguo alisema kwa kipindi kile viwango vya kubadilisha fedha vilikuwa ni tofauti, akitoa mfano wa mwaka 2009 kuwa Dola moja ilikuwa chini ya Sh1,000 lakini kwa sasa ni zaidi ya Sh1,800." chanzo.http://www.mwananchi.co.tz/habari/K...-tena/-/1597296/2642158/-/3b90tl/-/index.html

Mzizi Mkavu naona mizizi inakulewesha. Hii habari ililetwa na wenzio juzi usiku wewe leo ndo unanaona utoke nayo leo asubuhi. Wewe ni mzoefu sana wa mambo ya mizizi na sio ya biashara
 
Mzizi Mkavu naona mizizi inakulewesha. Hii habari ililetwa na wenzio juzi usiku wewe leo ndo unanaona utoke nayo leo asubuhi. Wewe ni mzoefu sana wa mambo ya mizizi na sio ya biashara

unaweza ukawa unashughulika na mizizi lakini kibiashara...kwenye magazeti mengi leo yameandika yashuka tena binafsi nilijua imeshuk tofauti na being niiyoisikua juzi....
 
Nina supply Diesel Door To Door kuanzia litre 200 na kuendelea DSM kwa Tsh 1,545 per litre,free transport.
0789 780 200
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…