Bei ya tikiti sokoni kwa sasa

kupigakazi

Member
Joined
Sep 17, 2014
Posts
53
Reaction score
10
Kwa wenye ufahamu kuhusu bei ya tikiti .Natarajia kuvuna tikiti mwezi huu wa tisa mwishon naomba kujuzwa being za masoko zikoje. Tafadhari kwa mwenye taarifa anijuze.
 
Aisee hongera,ni uwekezaji mzuri!
 
Ninavyo sikia kwa sasa bei mbovu sana .ndugu yangu amelima na anasema mwaka huu hasara
 
inauma sana wametunyima ajira tukaamua kulima nyanya kila mtu anajua kilichotokea tukakimbilia kwenye matikiti maji tena nakumbuka bikira wa kisukuma alianzisha kampeni kwa kushirikiana na vijana wakaenda kulima kwa nguvu zote lakin hata huku mikosni tulilima sana matikiti............ katika kujibu swali lako ndugu bei ya tikiti ni mbaya mno kuna mikoa unapata matikiti matatu kwa elfu moja
 
Jamani huko tuendako tunatakiwa tujigawe mfano huko Dumila Kilosa na kwingineko kabla ya kuanzisha mradi ufanyike utafiti wa masoko, Ma Dr. na Maprofesa msikimbilie siasa saidieni jamii katika hili,Wakenya wanasafirisha maua na mazao ya mbogamboga kwa ndege kwenda Nchi za Ulaya na hiyo ndiyo impact ya wasomi. Sisi tunajenga viwanja vya ndege vya kusafirisha abiria na madawa ya kulevya tu.Ndio maana nachelea kuingia katika kilimo cha mazao ya mbogamboga kwani huwezi kuhifadhi kwa muda mrefu,Aheri nilime mahindi na mpunga japo mbogamboga inalipa katika eneo dogo
 
Ninanunua almost kila wiki kwa dsm inaanzia buku 2, 3,4 na kubwa kabisa tano ..hiyo ni bei ya sokoni kama kkoo na masoko mengine..
 
Soko lipo la kutosha tatizo ni kuwa wote tunategemea soko moja tu lililopo Dar. Mfano ishu ya nyanya wakati Moro wakikosa wateja kuna mikoa bei bado IPO juu Na ni adimu.
 
Wale wajanja wa kilimo wao mwezi huu kiangazi kinapoanza kuwa kali wao ndo wameanza kulima. Wale walioingia sokoni miezi ya mwanzoni mwa mwaka wakakuta bei ya vitu viko juu. Alafu wakaamua kulima na bei ikawaporomokea kabla hata mazao yao kuiva. Umezamisha mil2 afu unakuta bei ni buku
 
Usitegeme Kama hao maprof na Madokta watatusaidia,kikubwa tuchakarike sisi wenyewe na kutafuta masoko,serikali yenyewe kupitia wizara husika wamelala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…