Bei ya ufuta

Jamani mbona ufuta mwaka huu bei ndogo sana leo kilo imefikia 1500 hapa Mpanda na Sumbawanga kuna nini safari hii
Huku dar kuna wanunuzi wananunua kwa 2250
Hata Ukiwa na mzigo mkubwa
 
ni kweli umeshuka bei mwaka huu. RUFIJI 1700/=. LAKINI HAO WANAONUNUA WANAKUJA KUUZA DAR KWA HIYO BEI YA 2250/= HIVYO NI HAKI YAO KUNUNUA 1500/= KWA SUMBAWANGA. KUMBUKA MWAKA HUU UFUTA UMEKUBALI SANA, KARIBIA SEHEMU ZOTE ULIOLIMWA UMEZAA VIZURI HIVYO NI MWINGI SANA NDIO MAANA BEI IMESHUKA. USIKATE TAMAA NDIO KILIMO CHA TANZANIA
 
Huku dar kuna wanunuzi wananunua kwa 2250
Hata Ukiwa na mzigo mkubwa

Hiyo bei anayosema ni manunuzi kwa Mpanda sasa nafkiri akiisafirisha mpaka ikifika sidhani kama itabaki kuwa bei hiyo hiyo.

Na pia mi nadhani ni vyema wangejaribu kupata soko la kimataifa kwa kupata connection toka kwa baadhi ya watu tofauti ila kuna changamoto zake pia lakini wakifanikiwa kupata faida yake ni nzuri sana.

Niliona uzi hapa kama siku mbili tatu hivi nyuma kuna mtu ana TANI 50 za ufuta sasa kwa kiasi hiko kama ukiuza kwa hapa nyumbani na ukiuza nje ya hapa faida yake haiwezi kuwa sawa................ONGEZENI SPEED MUWAHI KUFIKA.
 

hapo rufiji kwa maana ya ikwiriri na nyamwage ufuta haujakubali sana ni wachache wametusua wengi umeharibika kwa kuchelewa mvua na tatizo la wadudu. uko rufiji gani?
 
Kwa huku dar soko la uhakika lipo wapi/wanunuzi wapo wapi wenye kununua ufuta kwa haraka na kwa bei nzuri?
 
Bei ya ufuta imezidi kushuka ktk soko ndugu zanguni, kama kawaida ya biashara kwanza supply imekuwa kubwa sana, Rufii kwa leo kwa maana ya Bungu, kwa Msafiri, bei Tzs 1400 kwa kilo moja, na hata Dar es salaam bei sio stable sana hii imefanya baadhi ya watu kuweka stock katk majumba yao, hivyo wenye mzigo ngoma iko wazi hiyo kusuka au kunyoa bei bado mtu asije akukundaganya kuwa iko juu si kweli tegemea kushuka tena ndani ya siku 2 u week,
Jamani mbona ufuta mwaka huu bei ndogo sana leo kilo imefikia 1500 hapa Mpanda na Sumbawanga.

Kuna nini safari hii
?
 
mimi nahitaji kununua kama tani mbili hivi... mtoa mada unaweza kunitafutia hizo tani fasta fasta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…