God is Dead
JF-Expert Member
- Jan 11, 2019
- 1,311
- 1,533
Kazi ya mkulima inaishia kwenye kukata kitunguu kuanzia kuchambua kugonga na kupakia hiyo ni kazi ya mnunuziNimekuelewa.
Lakini hujanijibu.
Ni kwamba vitunguu unachukulia shambani maana yake wanachambua wanapakia kwa gunia unaona au ubakuta tayari gunia wanakuambia hii grade 2 sh kadhaa.
Cha msingi uwe na dalali wa kukutafutia kitunguu kila gunia utampa 3000Hayo mashamba ukifika tu unapata au ndo ya kutafuta? Maana unaweza kuta mashamba kumbe kuna watu waliwekeza hela zao au wana wateja wao.
Ahsante sana kwa maelezo haya.Kazi ya mkulima inaishia kwenye kukata kitunguu kuanzia kuchambua kugonga na kupakia hiyo ni kazi ya mnunuzi
Huwa magari yanaingia mpaka shambani na ikiwa kuwa gari haliingii mnunuzi na mkulima watachangia hasara ya kupeleka kitunguu kwenye gari
Ahsante.Cha msingi uwe na dalali wa kukutafutia kitunguu kila gunia utampa 3000
Siku hizi hakuna wakenya wanaoingia soko la kilombero kununua vitunguu, wakenya wanaenda shambani moja kwa moja mang'ola kununua, hapa kilombero wanunuzi ni wamama na wafanyabiashara wengine wanaopeleka kwenye masoko ya ngaramtoni, usa river, sadala nk. pamekua pa tofaut sana kilombero sio kama zamani biashara ilikua inafanyika kwa cash siki hizi ni mkopo unapeleka mzigo pesa utaipata baada ya wiki moja au zaidi.Ni shambani ndo wanachukulia mara nyingi , ingawa kwa Arusha kuna soko la vitunguu linaitwa Kilombero , sasa huko ni Wakenya na wenye mitaji mikubwa ndo wanaenda chukua mzigo , Ila ukitaka kupata mzigo nzuri nenda shambani Mang'ola
Kuhusu suala la kuchambua ni gharama ya mnunuzi kiufupi gharama ziko hivi ( vifungashio + gharama ya vibarua kuchambua , kulalia kwenye magunia , kupandisha kwenye gari + gharama ya usafiri + ushuru ) .
Tractor gunia moja huwa ni 2000Ahsante.
Nina swali mfano unataka kuchukua gunia 10. Maana yake hizo gunia hakuna uwezo wa kukodi gari nzima. Suala la usafiri kutoa shamba mpaka main road kusubiria gari inakuwaje?
nilikua hapo jumamosi grade one ilikua 110,000 mpk 120,000Anhaa basi nilikuwa sijui , nina siku nyingi sijaingia humo sokoni