Bei ya Vitunguu yapaa kufikia Tsh. 450,000/- kwa gunia soko la kimataifa Singida

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
BEI YA VITUNGUU YAPAA, GUNIA LAUZWA 450,000 SINGIDA

Bei ya vitunguu katika Soko la Kimataifa la Misuna lililopo mjini Singida limeendelea kupanda ambapo gunia moja la kilo 100 linauzwa kwa shilingi 450,000 kutoka shilingi 250,000.

AzamTv

 
wacha wakulima wafaidi.vp kwenye gunia ya kl 100 kwa wastani zinaingia vitunguu vingapi
 
Kitunguu kimoja hadi Tsh 800, Kisado wanazua elfu 18.
 
Unafkiri vitachambuliwa jui?! Au haujawahi kuona jinsi vitunguu na mang'ana hutenganishwa?!
Nisaidie, mang'ana ni nini?na ni lazima wachambulie sokoni?

Angalau wangejenga sakafu iliyonyanyuka maana hili soko kipindi cha mvua maji na tope hujaa na vitunguu huoza mara kadhaa nimewaona kwenye vyombo vya habari wakilalamika.

kifupi hili soko ni uwanja tu hata sehemu ya kujikinga mvua na jua hamna,hamna uzio,Hadhi ya Kimataifa halina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Of course ni uwanja wenye office za soko na vyoo napafahamu vizuri sana
Niliskiaga wanataka weka soko lakisasa sjui iilikshiaga wapi
 
Innocent Bashungwa come this way......

Usisahau kuwa miomgoni mwa tiba mbadala za covid19 ni kitunguu maji, sasa sie tia maji tia maji wa betri low tukikosa kitunguu ndani idadi ya vifo vya matatizo ya upumuaji itaongezeka sana.

NB: MNAOJUFUKIZA TUMIENI NA VITUNGUU NI DAWA YA MIAKA MINGI YA MAFUA NA KIFUA..
 
Ni kweli Dodoma Jana nimeona vitunguu 3 vinauzwa 1000/!
Nafikiri mvua kubwa zilizonyesha zimesababidha upungufu huu,
 
Hehehe...betri low
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…