Anna Nkya
Member
- Oct 21, 2021
- 69
- 341
Tangu mwishoni mwa Novemba mwaka jana, baada ya gazeti hili kutoa taarifa za kupanda kwa bei ya bidhaa hizo na zile za ujenzi, bei za vyakula zimepanda tena katika mikoa mbalimbali, huku Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akisisitiza Taifa kutokuwa na uhaba wa chakula, na kwamba ongezeko la sasa la bei, halina uhusiano na ukame kama inavyodaiwa na baadhi ya wadau waliozungumza na Mwananchi.
Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipotahadharisha kuhusu matumizi yasiyo ya lazima ya nafaka, akisema kutakuwa na upungufu kidogo wa chakula.
Akizungumza katika tamasha la utamaduni lililofanyika mkoani Kilimanjaro Januari 22, Rais Samia alisema:
“Niwaombe wakazi wa Kilimanjaro tupunguze kidogo matayarisho ya mbege na vinywaji vingine kwa kutumia nafaka zetu. Tujue kwamba mwezi wa 10 hatukupanda, tutapanda mwezi wa tatu na tutakuwa na upungufu kidogo wa chakula. Tutumie chakula kidogo tulichonacho ili kije kutufaa huko mbele,” alisema, huku akisisitiza kuwapo kwa akiba ya kutosha ya chakula nchini.
Naye Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji katika mazungumzo na watumishi wa wizara hiyo Januari 18, 2022, aliipa siku tatu kutoka siku hiyo Tume ya Ushindani (FCC) kutoa sababu za kuadimika kwa vinywaji baridi sokoni pamoja na kupanda kwa bei ya vifaa vya ujenzi.
Akizungumza juzi kwa simu na Mwananchi, Mtendaji Mkuu wa FCC, William Erio alisema walipokea maagizo ya waziri na wanayatekeleza kama alivyoelekeza.
“Kwa hiyo tukimpelekea taarifa atazipitisha kwa wasaidizi wake wazipitie na wamshauri. Kupitia ushauri huo atajua kipi aueleze umma, kwa hiyo sisi tutaripoti kwake kama alivyosema siku ile,” alisema Erio.
Hali ilivyo sokoni
Uchunguzi wa Mwananchi hadi juzi Ijumaa, umeonyesha kuwapo kwa ongezeko la kimya kimya la bei za vyakula katika maeneo mbalimbali nchini.
Kwa mfano, jijini Mwanza bei ya kilo moja ya mchele ambayo miezi miwili iliyopita ilikuwa ikuzwa kwa Sh1,200 imepanda hadi kufikia wastani wa kati ya Sh1, 500 hadi Sh1,800 kulingana na ubora.
Maharagwe pia yamepanda kutoka Sh2,000 kwa kilo hadi Sh2,200, huku bei ya kilo moja ya nyama nayo ikipanda kutoka Sh7, 500 hadi Sh8,000 au Sh9,000.
Mjini Shinyanga bei ya jumla ya mfuko wa sukari wenye ujazo wa kilo 50 unauzwa kwa Sh122,000, huku kilo moja kwa rejareja ikiuzwa kwa Sh2,800 kulinganisha na bei ya awali ya Sh2,600.
Kilo moja ya unga wa sembe imepanda kutoka Sh800 hadi kufikia Sh1,100, huku kilo moja ya mchele ambayo awali ilikuwa inauzwa kati ya Sh1,400 hadi Sh1,500 sasa inauzwa kati ya Sh1,600 hadi Sh2,000 kutegemeana na ubora.
Jijini Mbeya katika soko la Sido bei ya mchele, imepanda kutoka Sh40,000 mpaka Sh45,000 kwa gunia la kilo 100 kulingana na ubora, huku mahindi yakiuzwa kwa bei ya Sh13,000 mpaka Sh14,000 kwa ujazo wa kilo 20.
Mfanyabishara wa mchele katika mashine za kukoboa mpunga, Mwanne Joseph alisema kuwa huenda bei ya vyakula ikaongezeka kutokana na baadhi ya wakulima msimu uliopita kuuza kwa bei ya hasara na sasa hali ya ukame umechangia mfumuko huo.
Mkoani Dodoma pia kumekuwa na ongezeko la bei za vyakula. Katika soko la Majengo, bei ya mchele imeongezeka hadi kufikia 1,700 kwa kilo ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo kilo iliuzwa hadi kuanzia Sh1,300.
Jijini Arusha nako bei za vyakula zimepanda. Kwa mfano, mchele na unga vimepanda kati ya Sh1,000 hadi Sh3,000 kwa kilo moja.
Mfanyabiashara wa duka la rejareja mkoani Kilimanjaro, Hamis Issa alisema unga wa dona uliokuwa ukiuza Sh800, sasa unauzwa Sh1,000, huku sembe iliyokuwa ikiuzwa kwa Sh1,000 kwa kilo, sasa ni Sh1,200. Mchele ulikuwa ukiuzwa Sh2,000, na kwa sasa umepanda hadi kufikia Sh2,400.
Muuza nyama katika soko la kati, Manispaa ya Moshi, Hussen Iddi alisema nyama imepanda kutoka Sh8,000 kwa kilo hadi kufikia Sh9,000.
Mkoani Mtwara, baadhi ya wafanyabiashara wa vyakula walisema ongezeko la bei za vyakula linatokana na hali ya ununuzi kutoka maeneo ambayo wananunulia bidhaa hizo.
Hamis Mtende, anayefanya biashara katika soko kuu la Mtwara alisema kuwa kwa sasa hakuna mchele wa Sh1,000 hadi Sh1200, bali sasa unaanzia Sh1,900 hadi Sh3,000, karanga zilikuwa zinauzwa kwa Sh3,000 lakini sasa zinauzwa Sh4000, unga wa sembe kilo tano kutoka Sh7,000 hadi Sh10,000.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Mtwara, Hamza Licheta alikiri kupanda kwa bei za vyakula, huku akitoa mfano wa kiroba cha unga wa dona kilichokuwa kikiuzwa kwa Sh14,000, lakini sasa kinauzwa kwa Sh20,000 na kiroba cha unga wa sembe kutoka Sh18,000 hadi Sh25,000.
“Unajua kupanda kwa bei kumeathiri hadi nyanya; zamani kilo 30 tulikuwa tunanunua kwa Sh25,000 lakini leo hii tunanunua 45,000,” alisema.
Baadhi ya wafanyabiashara wa vyakula jijini Dar es Salaam walisema ongezeko la bei za vyakula limesababishwa na upungufu wa mvua za mwaka.
“Sababu ya kupanda kwa bei ya mazao ni kuchelewa kwa mvua, ndiyo sababu kubwa. Siyo kwamba itachukua muda mrefu, tutegemee watu wakijiandaa mpaka Julai, vyakula vitakuwa tayari, lakini kuanzia mwezi huu hadi Juni, bei haitashuka bali itazidi kupanda zaidi,” alisema Shebughe Mndolwa, anayefanya biashara katika soko la Kisutu.
Hata hivyo, alisema kuna baadhi ya wafanyabiashara wenye tamaa wanaoficha bidhaa wakati wa shida na kuongeza bei.
Wasambazaji wa vyakula
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya kampuni za usambazaji wa chakula zimeeleza sababu ya ongezeko hilo, ikiwa pamoja na ukame na gharama za usafirishaji.
“Jibu rahisi ni ukame,” alisema Said Makilagi ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Musoma Food Company Limited inayosambaza nafaka ndani na nje ya nchi.
Aliendelea: “Kwa kawaida mvua inaanza kunyesha Oktoba kuja Novemba na kuendelea, lakini haikunyesha, kwa hiyo hakukuwa na uzalishaji. Hata hii mnvua inayonyesha sasa haitasaidia kitu.”
Alisema kutokana na hali hiyo bei ya mazao imepanda kwa wakulima na ndiyo maana hata kwa wauzaji wa rejareja imepanda.
“Tutegemee bei kupanda mara mbili zaidi, kwa sababu hakuna chakula,” alisema.
Hata hivyo, kwa upande wake alisema bado wanaruhusiwa kusafirisha chakula nje ya nchi... “Hatujazuiwa kuuza chakula nje ya nchi, ndio maana tunaendelea kuuza.”
Kwa upande wake, Hussein Sufian ambaye ni Mkurugenzi wa habari na uhusiano wa kampuni ya Bakhresa, alisema kiini cha bei hizo ni kupanda kwa gharama za usafirishaji.
“Sisi tunafanya biashara ya ngano, tunanunua kidogo hapa nchini na nyingine nje ya nchi. Kuna ongezeko la gharama za usafirishaji kutoka nje ya nchi na usafirishaji wa ndani, ndiyo maana hata bei zinapanda.
“Siyo kwamba kuna ongezeko la mahitaji, isipokuwa ni gharama za usafirishaji na kupanda bei kwa mazao ya kilimo,” alisema Sufian.
Taarifa ya Wizara
Kwa mujibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, bei za bidhaa za vyakula, hususan nafaka zote zimeonekana kuongezeka katika kipindi cha kutoka Januari 2022 ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Bei hizi zinajumuisha nafaka muhimu aina saba na viazi mviringo. Haya yameonekana kupanda bei isipokuwa maharage yaliyoshuka kidogo.
Bei ya gunia la mahindi ilipanda kwa asilimia 27 na kufikia wastani wa Sh70,732 kwa gunia la kilo 100 ilipofika Januari 27 mwaka 2022 na Sh55,871.3 Januari 28, 2021.
Gunia la kilo 100 la mchele limepanda hadi Sh207,058 ukilinganisha na wastani wa Sh162,77.8 katika kipindi hicho, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 27.
Bei ya gunia la ngano imefikia Sh149,090.9 kutoka wastani wa Sh88,230 na Sh108,125 katika kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Uwele na ulezi vimeongezeka hadi kufikia wastani wa Sh128,909 na Sh179,285 kwa gunia la kilo 100 kutoka Sh97,700 na Sh144,812 katika kipindi kama hiki mwaka 2021, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 32 na asilimia 24 mtawalia.
Viazi mviringo vimeonyesha ongezeko dogo la asilimia tatu, huku vikiuzwa kwa wastani wa Sh83,100 ukilinganisha na Sh80,970.6 mwaka uliopita.
Maharage ndiyo nafaka pekee iliyoshuka bei kwa kiasi cha asilimia nne.
Gunia la maharage limepungua kutoka wastani wa Sh210,666.7 hadi Sh203,235.3 katika kipindi hicho.