Wadau naomba mnipe mawasiliano ya mtu anayeuza filter za kusafishia maji ya kisima yenye chumvi pamoja na wireless router za cmu ni mhm n nmeona jamiiforums ndo duka pekee ambalo najua hakishindikani kitu
Hapo kwenye blue,
Kama uku Dar, watafute Merry Water (wako eneo la Victoria barabara ya Bagamoyo kama unatoka city center Dar kwenda Mwenge).
Pia watafute Davis & Shirtlif (wako eneo la Kamata, karibu na Kariakoo).
mkuu nenda ardhi university,ili upate salinity content ni kiasi gani,afu ndio upeleke merry water hiyo specs,pia kuna muhind flan yupo hapa mitaa ya samora avenue,yeye anapima mwenyewe na kukupa filter,kama chumvi sio nying lakini,bei yake si chini ya laki 8.