Bei za kuruka ni hasara kwa serikali na wanunuzi

Bei za kuruka ni hasara kwa serikali na wanunuzi

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Mdau wa Jamiiforums ameandika, Waziri wa Kilimo Joseph Hasunga amesema viwanda vyote huwa vinasimamisha uzalishaji mwezi Mei ili kufanya ukarabati, mwaka vimesimamisha miezi miwili kwa sababu mashamba ya miwa yamejaa maji na ndio sababu ya sukari kupanda bei.

Kutokana na tabia ya kutodai risiti bei hizi za kuruka ni hasara kwa wanunuzi na serikali. Kwa wanunuzi, wanapata maumivu kwa kuwa wanatumia hela nyingi kununua bidhaa ambayo mwanzo ilikuwa ni ya bei ndogo, kama sukari kutoka bei elekezi ya Tsh 2,200 hadi 4,500.

Wafanyabiashara wengi wanaouza sukari kwa kupimiana kwenye maduka yasiyo ya jumla hawatoi risiti. Hali inayofanya mtu alipe bei kubwa lakini Mamlaka ya mapato itashindwa kukadiria kodi ipasavyo kwa kuwa hakuna risiti ya kuonyesha ongezeko la thamani (VAT)

Hapo hasara inakuwa kwa serikali kwa kuwa wanakosa kodi stahiki, na kwa wanunuzi ambao wanatoa hela iliyozidi. Hapo mfanya biashara ataendelea kupata faida mara dufu huku wengi wakiumia.

Tabia ya kutotoa na kutodai risiti ni sababu kubwa, lakini pia serikali ikiingilia kati itasababisha bidhaa husika ziwe kimagendo zaidi na ikose hata kidoogo kinachopatikana.

Kama tutaamua kuacha nguvu ya soko iendelee kufanya kazi basi mnunuzi ataumia haswa.

Ushauri: Tukipita hili janga tuangalie namna tunavyopoteza hela kwa kuwa na mifumo mibovu ya kodi, mipango inahitajika

2. EFD ziangaliwe kwa namna ya kumsaidia mfanyabiashara, pia elimu ya kodi iwe swala endelevu, japo bado ukwepaji kodi hautaepukika kutokana na hali ya fulani fulani nchini kwetu ila tunaweza punguza.


====

Signed

Oedipus
 
Back
Top Bottom