Bei za mafuta zashuka kwa kiwango kikubwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) nchini Tanzania imesema, bei ya mafuta ya taa, petrol na dizeli zimepungua kwa baadhi ya mikoa kuanzia leo Jumatano tarehe 6 Mei 2020.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godfrey Chibulunje amesema bei za jumla na rejareja za mafuta ya petroli, dizelina na mafuta ya taa yaliyopokelewa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 1 Aprili 2020.
Amesema kwa Mei 2020, bei za rejareja za petrol imepungua kwa Shilingi 219/lita (sawa na asilimia 10.50), dizeli Shilingi 143/lita (sawa na asilimia 7.17) na mafuta ya taa yakipungua kwa Shilingi 355/lita (sawa na asilimia 18.47), mtawalia.
Kwa maana hiyo, Dar es Salaam petrol inauzwa kwa Shilingi 1,868, dizeli Shilingi 1,846 na mafuta ya taa Shilingi 1,568.

Chibulunje amesema bei za jumla za petrol imepungua kwa Shilingi 218.59/lita (sawa na asilimia 11.14), dizeli kwa Shilingi 142.25/lita (sawa na asilimia 7.63) na mafuta ya taa zimepunguakwa kwa Shilingi 354.09/lita (sawa na asilimia 19.69).

Amesema bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli katika mkoa wa Tanga zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 1 Aprili 2020.

Amesema Mei 2020, bei za rejareja za petroli na dizeli kwa mikoa ya Kaskazini (yaani Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara) zimepungua kwa Shilingi 463/lita(sawa na asilimia 21.88) na Shilingi 377/lita (sawa na asilimia 18.21),mtawalia.

Aidha, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za petroli na dizeli zimepungua kwa Shilingi 461.82/lita (sawa na asilimia 23.19) na Shilingi375.82/lita (sawa na asilimia 19.33).

Bosi huyo wa Ewura amesema bei za mafuta ya taa kwa mikoa ya Kaskazini zitaendelea kuwa zile zilizochapishwa katika toleo la tarehe 1 Aprili 2020 kwa sababu hakuna shehena ya bidhaa hiyo iliyopokelewa nchini kupitia bandari ya Tanga kwa mwezi Aprili 2020.

Kwa mwezi Mei2020, bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya dizeli katika mikoa ya Kusini (yaani Mtwara, Lindi na Ruvuma) hazitabadilika ikilinganishwa na toleo lililopitala tarehe 1 Aprili2020 kutokana na kuwa hakuna shehena ya dizeli iliyopokelewa kupitia bandari ya Mtwara.

Hata hivyo, bei za mafuta ya petroli zimepungua ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita.

Kwa mwezi Mei 2020, bei za jumla na rejareja za petroli zimepungua kwa Shilingi 129/lita (sawa na asilimia 5.67) na Shilingi 128.14/lita (sawa na asilimia 5.99).

Kwa kuwa hakuna Mafuta ya Taa katika bandari ya Mtwara, wamiliki wa vituo vya mafuta katika mikoa tajwa wanashauriwa kununua mafuta hayo kutoka Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa kwa mikoa hiyo zinatokana na gharama za mafuta hayo kutokea Dar es Salaam na kusafirishwa hadi mkoa husika.

“Mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la ndani yanatokana namabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia na gharama za usafirishaji (BPS Premium),” amesema Chibulunje

Kuangalia bei zote za mafuta katika sehemu zote nchini, bofya pdf chini
 

Attachments

SAFI SANA, TUNAWASHUKURU VIONGOZI KWA KUSIMAMIA MAFUTA YASHUKE BEI MAANA WAFANYA BIASHARA WASIPOSIMAMIWA HATA KAMA HUKO NJE YAKISHUKA PENGINE WAO WAUZAJI WANGEENDELEA NA RATES ZA ZAMANI NA KUPIGA HELA.

SHUKRAN NA PONGEZI KWA VIONGOZI WETU.
 
Iwaje Arusha mafuta yawe chini zaidi ya Dar
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kadri marekani wanavyozidi kutandikwa na Covid19 ndio kadri ambavyo tabasamu langu linaongezeka kila nikifika sheli 🤣🤣🤣

What a goaal??? What a wonderful goal man! Marvelous win!

Hatimae almost litre 6 nazipata kwa sh.10,000 🤣🤣🤣🤣 tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…