Bei za vifurushi za bima ya afya ya NHIF vimebadilishwa. Gharama zimepanda

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Shirika la Taifa la Bima NHI hivi karibuni limebadilisha bei na majina ya vifurushi vyake.

Mabadiliko haya yalitangazwa tangu December 17th 2024 na sasa umepita takriban mwezi mmoja tangu mabadiliko hayo yafanyike.

Badala ya bei ya Tshs 194,000 sasa vifurushi vitaanzia 240,000 kwa watu wazima ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.76

Tunakumbushana tu kuwa juzi juzi hapa CCM walionesha mabasi yao ya kijani ambayo yalikuwa ni mamia kwa mamia.

Kwa hiyo pesa za kununua mabasi zipo ila pesa za kuongeza kwenye mfuko wa bima ili kumpa mwananchi unafuu katika huduma za afya hamna.

Soma pia: CCM wanatoa wapi fedha za kununulia msululu huu wote wa Mabasi, kama sio Kodi za Wananchi ni nini?






 
Hela zimekwenda kwenye heka heka za uchaguzi... Kule CDM kambi ya Mbowe wanatembeza hela kama njugu tu.
 

pesa za kuchezea kwenye siasa zipo. Za mambo ya msingi hazipo. Tunawahitaji kina Traore wengi humu shithole countries.

Jesus is Lord&Savior
 
Kitu ambacho huwa kinanishangaza nikuona bei za vifurishi ni kubwa kwa wazee ambao kikawaida tunaita wastaafu kuliko vijana wafanyakazi.
 
Ovyo Kabisa.
afya za watu kwao sio za msingi kabisa.
.Hiyo ghalama kwa mwanachi wa kipato gani anaweza kumudu?
.Kwa wabeba zege nk wataweza kumudu hizo ghalama kweli?
.
 
Shauri yao, Mwamposa yeye hatibu kama zinavyofanya hospitali, yeye anaponya.
 
INNA LILAH WAINNA ILAIH RAGIUN msiba mkubwa huu
 
Ni hatari sana. bi mkubwa nilikua namlipia 360,000 saivi inabidi nilipe 708,000 .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…