Beki bora wa Tanzania miaka ya nyuma ni nani?

Paul John Masanja(yanga Fc) Na Victor Costa(simba) enzi zao hawa ilikuwa shughuli
 
Kikosi kazi cha ukuta wa berlin ni iki hapa taifa stars: 2.mohamed mkweche 3. Daud salum "bruce lee" 4. Leodgard tenga "msomi" 5. Jela mtagwa .......... Golini alikuwa juma pondamali "mensah"athuman mambosasa ilikuwa ya uhakika

jela mtagwa "alistaili fifa fair player" alikuwa beki mstaarabu sana
 
Mkuu,

Said Mwamba "Kizota" alikuwa mshambuliaji, siyo beki kama mada inavyosema!

Nilijua tu kutatokea raia kama wewe...

Marehemu Kizota kabla ya kuwa mshambuliaji hatari alikuwa akicheza centre half (beki wa kati)...

Nadhani sasa utajua kwa nini nimeliandika jinale....
 
Nilijua tu kutatokea raia kama wewe...

Marehemu Kizota kabla ya kuwa mshambuliaji hatari alikuwa akicheza centre half (beki wa kati)...

Nadhani sasa utajua kwa nini nimeliandika jinale....

Uko sahihi mkuu. Hata baada ya kuwa mshambuliaji mara kadhaa alicheza kama beki na kung'ara.
 
Sijui kuhusu Ubora kuliko wote.., lakini katika uniqueness, Beki Mstaarabu Ayubu Mzee..., jamaa alikuwa hachafuki anatoka uwanjani jezi bado safi kama ndio anaingia....

Ila katika Mabeki duniani kote ambaye nina uhakika angefika mbali na alikuwa na akili sana na Ball Control na kujiamini ni Marehemu Eston Mulenga..., huyu jamaa alikufa na ile ndege iliyowauwa Zambia.., jamaa alikuwa hana papara striker ukija anakunyanganya mpira unapigwa chenga alafu anaanzisha move.... Simply Brilliant...
 
keysersoze huyo beki aliitwa samli ayubu alikuwa maji maji na kina Peter muhina na abdul ntila golini alikuwa isihaka majaliwa.
 
Leopold Mukebezi Tasso - Balimi / TAIFA STARS
 


  • Frank Kassanga Bwalya......Simba SC
  • Mustafa Hozza.........Simba SC
  • Jamhuri Kihwelo........Simba SC
 
Beki kisiki aliye dumu sana ktk timu ya taifa alikuwa Mohammed Chuma. Huyu alikuwa chinga kama kumbukumbu zangu ziko sahihi alikuwa akichezea timu ya bandari Mtwara.
 
Baba yangu alinambia anaitwa Chuma anatokea Mtwara hakucheza Yanga wala Simba yeye ni Taifa Stars tu akimaliza anarudi mtwara na alistaafu kwa heshima.
 
Muhidini Cheupe Yanga & A. F. C
Kimune Mwita Simba& AFC
Twaha Hamid Simba
Kasongo Athumani Simba
Kenneth Mkapa Yanga


Mabeki bora simba; Shaaban Baraza, Shaaban Baraza(1972-1975),Mohamed Kajole( 1971…-1980),Arthur Mambeta ….1973, Omari Chogo(1972-1975), Aloo Mwitu 1974-198….,AthumaniJuma 1974-198…,TALL 1975 -1978/9, Daudi Salum(Bruce Lee) 1976-1980, Deo Njohole……1989……wenginena yanga nitaendelea baadaye
Mabeki wa siku hizi ingekuwa zamani wangekaa benchi mpakawanastaafu e.g. CANAVARO….
 

Mkuu, beki mstaarabu alikuwa Samli Ayoub sio Ayoub Mzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…